Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa Bunge Maalumu la Katiba litaanza
Februari 18 mwaka huu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini
kuweka mbele masilahi ya Taifa na siyo ya vyama vyao.
Rais Kikwete alisema wajumbe 640 wa Bunge hilo wengi ni wafuasi wa
vyama vya siasa, hivyo wanatakiwa kukubaliana kwa hoja badala ya kila
upande kuvutia kwake.
Msichana aliyebakwa na genge la watu sita nchini Kenya hatimaye huenda akapata kutendewa haki.
Liz mwenye umri wa miaka 16, alibakwa na
kujeruhiwa vibaya mwezi Juni baada ya kutupwa ndani ya shimo la choo
katika jimbo la Busia Magharibi wma Kenya.
Maelfu ya waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakiondoka katika mji mkuu wa taifa hilo Bangui mapema leo.
Wakiwa wameabiri malori na kusindikizwa na
wanajeshi wa taifa la Chad,ni msafara wa hivi karibuni wa waislamu
kutoroka vita wakiwa na matumaini ya kupata hifadhi katika taifa jirani
la Chad.
Serikali imekanusha taarifa za vyombo vya
habari zilizodai kuwa wabunge wa nchi hiyo watalipwa kiasi cha zaidi ya
dola laki moja za kimarekani watakapomaliza muda wao wa kipindi cha
miaka mitano yakiwa malipo ya #kiinua_mdomo.
Taarifa ya wizara ya fedha imesema habari hiyo
ni ya upotoshaji kwa kuwa Waziri wa fedha ,hakuwahi kuzungumza na
mwandishi yeyote kama inavyodaiwa kuwa alithibitisha taarifa hizo.
Mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya amewaomba radhi
wanawake kwa matamshi yake wiki jana kuwa wanawake ambao hawajaolewa
hawapaswi kushikilia nyadhifa za kisiasa.
Gavana wa kaunti ya Kiambu nje kidogo ya
Nairobi, William Kabogo, amesema kuwa ikiwa wanawake wana umri wa miaka
35 na bado hawajaolewa basi wao sio timamu.
Kiongozi wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila
amenusurika kifo na mtu mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la
Mikidadi, ambaye yupo mahututi katika Hospitali ya Temeke, baada ya
kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa na mzozo wa ardhi eneo la Kurasini,
jijini Dar es Salaam.
WAKATI watumishi wa umma wakitaabika na mishahara midogo, huku wakipendekeza marupurupu ya wabunge yapunguzwe, wabunge wa CCM juzi waliwaweka kitimoto viongozi wa Bunge wakitaka mishahara yao ipandishwe.
Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa,Aliwataja wafuasi waliouawa kuwa ni Ramadhan Hamis, ambaye ni mfanyabiashara wa madini na mwingine jina lake halikufahamika mara moja lakini inasemekana ni mwalimu wa dini ya Kiislamu (ustaadh) Kijiji cha Lwande.
Leo katika kikao cha kawaida cha kupeana taarifa za mambo mbalimbali ya bunge, wabunge wamemjia juu Spika Anna Makinda na Naibu Spika wake Ndg Job Ndugai wajiuzulu kwa kushindwa kusimamia kanuni ipasavyo na pia kwa kushindwa kusimamia maslahi ya wabunge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, leo wamehudhuria msiba wa baba yake na muigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu, Balozi Abraham Sepetu aliyefariki jana baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya kisukari na kiharusi. Alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam..
Viongozi wa dini wametaja majina 61 ya vinara wanaojihusisha na dawa za kulevya nchini ambao wanatarajia kuwaburuza katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kujibu tuhuma zao.