MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamata magari 70 ya abiria kutokana na kufanya makosa mbalimbali.
“Tumegawa chati za bei kuanzia Jumatatu kwa kila gari, zenye utambuzi wa bei ya nauli za zamani na mpya hivyo kila mwananchi anayo haki ya kuoneshwa chati hiyo pindi anapotaka na akinyimwa kuiona hilo ni kosa na mhusika atachukuliwa hatua,” alisema Shio.
Alisema mamlaka hiyo pia itakamata madereva ambao wataendesha magari ambayo hayajafuta bei ya zamani ubavuni mwa magari yao na magari yote yatakayokamatwa kwa makosa mbalimbali yatawekwa katika yadi ya mamlaka hiyo na kusubiri uamuzi wa mkurugenzi kama atayafuta kabisa au la.
Alisema nia ya mamlaka hiyo ni kuboresha hali ya usafiri katika kila pembe ya jiji ili kila abiria aweze kusafiri na kufika anakokusudia bila ya vikwazo vinavyotokana na tamaa za watu wasiotosheka na wanachokipata kihalali.
Pamoja na mambo mengine alisema hivi karibuni alikutana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani katika kupanga mikakati ya kuyakamata magari yote yaliyosajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma kati ya mikoa hiyo na kunyang’anywa leseni.
No comments:
Post a Comment