Takriban viongozi 160 wa kidini nchini Somalia wametoa kauli au Fatwa inayolaani kundi la al-Shabab, wakisema kuwa kundi hilo haliruhusiwi kabisa katika dini ya kiislamu.
Wadadisi wanasema kuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi wa kidini nchini Somalia kutoa Fatwa aina hiyo kulaani kundi hilo ambalo linadhibiti maeneo mengi ya vijijini na mijini.
Katika kongamano kuhusu tatizo la itikadi kali mjini Mogadishu, wasomi hao walisema kuwa wanalaani jambo la Al Shabaab kutumia ghasia kuwahangaisha wananchi.
Al-Shabab, au Vijana kwa maana nyingine, wanapigania kile wanachosema ni taifa la kiislamu.
Licha ya kuondoshwa katika maeneo ya mijini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kundi hilo bado linadhibiti miji midogo na sehemu kubwa ya vijijini.
No comments:
Post a Comment