
KABLA ya kwenda mbali ningependa kuungana kiroho na kihisia na ndugu zetu Waislamu wa Kenya katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na nnawaomba Waislamu wote wa Kenya wasichoke kupigania heshima ya Msikiti na Uislamu hata ikibidi kufa. Msiba uliowakuta unatuhusu sote kwa sababu ndugu wa Uislamu hautenganishwi na mipaka ya jiografia wala utaifa.
Tukio la polisi kuua Waislamu Msikitini limeshatokea hapa kwetu katika Msikiti wa Mwembechai jijini. Na makusudi ya makala haya kufanya ulinganifu jinsi tatizo hili lilivyopokelewa na kushughulikiwa hapa kwetu na huko Kenya. Nia na madhumuni yakiwa kuwaelimisha ummah wa Watanzania na watawala wao jambo sahihi la kufanya katika kuyashughulikia na kuepusha majanga ya namna hii.
Ulinganifu wa kwanza kabisa ungeanzia kwa serikali za nchi hizi mbili. Mara tu baada ya mauaji ya Mwembechai serikali ya Tanzania kupitia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Waziri wa mambo ya ndani ilieneza propaganda za ajabu dhidi ya Waislamu waliouliwa. Serikali ilikuwa inajaribu kuficha madhambi yake kwa kuonesha kwamba wale waliouawa na polisi walikuwa ni wahuni na wakorofi wachache. Wauaji hawakufikishwa mbele ya sheria na wangali wanalindwa na serikali yetu ya ukweli na uwazi.
Tofauti na serikali ya Kenya; kwanza hawakufanya propaganda za kuficha ukweli kwa kuwagawa Waislamu. Walijuwa ukweli hauwezi kufichwa kwa kutumia uwongo na Waislamu ni watu wenye kujitambua. Angalau waliona njia bora ya kushughulikia tatizo nyeti kama hili ni kuachia sheria ichukuwe mkondo wake. Kwa namna hii ndivyo inavyoweza kuulinda umoja wa kitaifa. Wamewafikisha mahakamani watuhumiwa wa mauaji ya Waislamu kama sheria na taratibu za nchi zinavyotaka. Somo gani tunalopata hapo?
Serikali yetu lazima ijifunze kuzingatia sheria na kanuni zilizopo ndani ya katiba katika kutatua mizozo inayohusu imani za wananchi. Kitendo cha polisi kuingia ndani ya Msikiti na viatu na kuua Waislamu kinavunja katiba ya nchi. Matumizi ya nguvu badala ya sheia kunazidisha chuki na uadui kati ya serikali na Waislamu. Serikali haitoweza kurejesha imani ya Waislamu iwapo wauaji wa Mwembechai hawatafikishwa mahakamani kama ilivyokuwa Kenya.
Halafu tukuchue Mabaraza Makuu ya Waislamu wa Kenya na Tanzania (BAKWATA na SUPKEM) tuyalinganishe katika kadhia hii. Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) liliungana moja kwa moja na serikali katika suala la Mwembechai. Yaani chombo cha Waislamu kinachopaswa kuwatetea na kuwasemea Waislamu wa Tanzania kiliunga mkono mauaji ya Waislamu pale Mwembechai kwa kukaa kimya katika tukio zito kama lile. BAKWATA iliisaidia sana serikali katika propaganda zake za kuwagawa Waislamu na kuwasambaratisha. Lakini SUPKEM ya Kenya ililaani vikali mauaji ya Waislamu ndani ya Msikiti wa Anas bin Malik na imesema si suala la watu kufikishwa mahakamani tu bali hatua kali zaidi zichukuliwe kwani kosa lililotendeka ni zito sana.
Katibu Mkuu wa SUPKEM Bw. Ahmad Khalif katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema kabla ya mauaji Msikiti umenajisiwa kwa polisi kuingia ndani na viatu na hivyo kuvunja heshima ya sehemu takatifu za ibada. Somo gani lipo hapo?
BAKWATA ambao wanadai ndiyo wenye mamlaka ya kisheria ya kusimamia masuala yote ya Waislamu wa Tanzania wamefanya dhulma kubwa sana kwa Waislamu kwa kukaa kimya wakati ambapo Waislamu walikuwa wanategemea msaada wao japo wa "kauli" tu ya kulaani mauaji ya Mwembechai. Kimya chao ndicho kilichoipa serikali kibri cha kufanya waliyoyafanya na kujenga mazingira mazuri ya kuwalinda wauaji. Waislamu wana haki na kila sababu ya kuikataa BAKWATA kwa jambo hili. Baraza gani hili linaloungana na maadui wa Waislamu kila Waislamu wanaponyanyaswa? Ni vyema BAKWATA likajifunza kutoka SUPKEM kwa kutoa kauli na misimamo inayowasaidia Waislamu. Kinyume cha hapo BAKWATA ni pango la adui wa Waislamu.
Baraza la Maimamu wa Kenya limeitaka serikali ya Kenya imfukuze kazi Mkuu wa Polisi wa Kwale Bw. David Kiarie. Baraza hilo pia limetishia kuitisha migomo ya wananchi wasusie shughuli mbalimbali za kiserikali iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa.
Maimamu wetu waige mfano wa Baraza la Maimamu wa Kenya. Baraza la Maimamu la Kenya linafanya kazi ya Waislamu. Mtume na Maswahaba hawajawahi hata siku moja kwenda kula futari katika Ikulu ya Abu Sufyan. Waislamu kamwe hawatawakubali Maimamu wasaliti. Wao ni maadui hatari zaidi kuliko wa nje.
Chama cha Wanasheria cha Kenya (The Law Society of Kenya) kililaani vikali mauaji ya Waislamu ndani ya Msikiti ambapo Mwenyekiti wake wa Tawi la Mombasa Bw. Stewart Madzayo amesema kuwa mauaji hayo ndani ya Msikiti yamekiuka sheria ya Jinai Kf. Na. 134..
Cha ajabu chama cha wanasheria wa Tanzania kilipiga kimya kabisa. Hakikuweza hata kutetea msimamo wa sheria na katiba katika sakata ya Mwembechai.
Bado tunakumbuka Wakili maarufu jijini alipojitoa kuwatetea Waislamu katika kesi ya mabucha ya nguruwe mwaka 1993 kwa hoja ya kuogopa kutengwa na Kanisa lake! Hawa ndiyo wanasheria wetu! Nini cha kuzingatia?
Wanasheria wa Tanzania kama wasomi waiokoe jamii ya Kitanzania kwa kutumia taaluma zao. Waache tabia ya kuendekeza ushabiki na ukereketwa usio na maana. Waige mfano wa The Law Society of Kenya ambao wametumia taaluma yao ya shreia kwa lengo la kuweka mambo sawa kwa manufaa ya Wakenya kama taifa.
Askofu Mkuu Ndingi Mwanaa' Nzeki amelionya jeshi la polisi juu ya hatua zake za kuvunja sheria na kuvamia Misikiti na Makanisa. Angalau Askofu huyu ameona ubaya wa vyombo vya dola kuvamia majumba ya ibada na kuua waumini. Lakini Kadinali Pengo aliunga mkono hatua ya polisi kumwaga damu za Waislamu katika Msikiti wa Mwembechai. Kadinali Pengo aliwalaani Waislamu waliouliwa Mwembechai kwa kuwafananisha na Goliath na wale polisi wauaji David! Yaani waliokuwa wanajitetea ni polisi waliokuwa wanashambulia ni Waislamu!
Cha kujifunza hapa ni kwamba viongozi wa dini lazma wazingatie haki na uadilifu. Wasilete batili hata kama inawasaidia kwa muda. Haki na usawa ndiyo msingi wa amani na utulivu wa taifa lolote lile. Wajuwe muundo wa jamii ya Kitanzania unatokana na watu wa dini mbalimbali. Hii siyo nchi ya Wakristo peke yao!
Waislamu wa Tanzania kama jamii lazima tuisaidie nchi kuepukana na wachafuzi wa amani. Waislamu watano wameuliwa ndani ya Msikiti na polisi lakini azma yao ya kulipiza kisasi kwa damu imesababisha serikali ya Kenya kumficha Kamanda wa polisi aliyeamuru mauaji yale
No comments:
Post a Comment