Friday, September 13, 2013

"omba omba " sasa kufukuzwa jijini dar es salaam...

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive, Dar es Salaam, imeamuru ombaomba zaidi ya 200 na watoto wao kurudishwa makwao na endapo watarejea watakwenda jela miezi mitatu. Amri hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Willium Mutaki baada ya kubainika kwamba walikuwa wakiomba katika maeneo ya wazi bila kibali.



“Mtarudishwa kwenu, mkirudi tutawapeleka gerezani miezi mitatu, msirudie tena kosa. Ofisi ya Ustawi wa Jamii ndiyo inashughulikia kuwarudisha, mtasindikizwa na usalama na kupokelewa katibu tawala wa mikoa yenu.

“Baada ya kupokea agizo kutoka kwa mkuu wa mkoa kuwa wakamatwe na kurudishwa makwao, hatua hiyo ilifanyika jana, ombaomba wanasababisha usumbufu, wanahatarisha maisha ya watoto wao wadogo na kuwanyima haki zao za msingi ikiwamo elimu,”alisema.

Akiwasomea mashtaka, Wakili wa Serikali, John Kijumbe, alidai Ester Shomi, watoto wake watatu na wengine zaidi ya 20, Septemba 11 mwaka huu walikutwa wakijiweka katika maeneo ya wazi jijini kwa nia ya kuomba fedha.

Ofisa wa Ustawi wa Jamii, Agnes Mbusa alidai washtakiwa walikuwa wakiomba fedha bila kibali.

“Ikiwezekana mheshimiwa Hakimu tunaomba mahakama itoe amri ya kuwarudisha makwao, utaratibu wa kuwarudisha umeshakamilika,” alisema Mbusa na kuongeza kwamba ombaomba hao wengi wametokea Dodoma.

No comments:

Post a Comment