Thursday, March 14, 2013

waislamu wapelekewa michezo buserere, lengo warudishe maridhiano na wakristo.


Shigongo akishirikiana na Mbunge wa Busanda-CCM,  Lolesia Bukwimba licha ya kukutanisha makundi yanayosigana pia waliandaa mashindano ya soka ili kuhamasisha amani katika eneo hilo.
Akizungumza  jana, Shigongo alisema kuwa wamefikia hatua kubwa katika utatuzi wao kwani viongozi wa dini hizo walifikia mwafaka na kusaini mkataba wa amani.
Katika vikao hivyo ambavyo viliwashirikisha Mbunge Bukwimba na viongozi wa Serikali Wilaya ya Geita, Mchungaji Isaya Ikiri na Sheikh Ismail Ibrahim waliwekeana saini ya makubaliano ya amani.
Shigongo alisema kuwa kati ya makubaliano waliyofikia pande hizo mbili ni kuwa Waislamu kuendelea kuchinja, lakini Wakristo wanaweza kuchinja lakini nyama yao isiingie katika biashara ya bucha.
“Pia pande zote mbili zimetakiwa kuwa makini, kwamba atakayekiuka makubaliano hayo kachukuliwe hatua za kisheria kama mtu binafsi na sio dini ihusishwe,” aliongeza Shigongo

No comments:

Post a Comment