Monday, November 12, 2012

nurdini kishki alivyodhalilishwa kwamba ni mhamiajii haramu

Shekhe Nurdin Kishki, alidai kusikitishwa na kitendo hicho ambacho pia kimewahusisha wageni wao kutoka nje ya nchi.

Akizungumzia tukio hilo, Shekhe Kishki, alisema msafara huo ulikuwa ukitoka Arusha na Tanga kwenda Dar es Salaam ukipitia njia ya Bagamoyo ili kuepuka foleni ya Barabara ya Morogoro.

Baada ya kufika Bagamoyo, walishangaa msafara wao ukisimamishwa na watu waliovaa kiraia wengine wakiwa na silaha.

Alisema baada ya kusimama, waliamuriwa kutelemka katika magari, kulala chini na kuwapekua wakipewa masharti mbalimbali na kutakiwa kutulia.

“Tuliwaeleza kuwa sisi ni mashekhe na tulikuwa tukitoka kwenye mikutano katika mikoa ya Arusha na Tanga, awali tulijua tumetekwa na majambazi lakini baada ya muda, tuligundua walikuwa polisi,” alisema Shekhe Kishki.

Aliongeza kuwa, polisi waliwapeleka Kituo cha Bagamoyo wakiwa chini ya ulinzi mkali kutokana na hisia ya msafara huo kuwa wa wahamiaji. 

Akizungumzia sakata hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo,  Ernest Mangu, alikiri kukamatwa kwa Waislamu hao ambao walikuwa wakitoka Tanga kwenda Dar es Salaam.

Alisema viongozi hao walikuwa na msafara wa magari mawili ambapo polisi wa doria waliwatilia shaka na kuwasimamisha ili kupata maelezo yao lakini walipotakiwa kusimama walikaidi.

Mkuu wa Mkoa huo Bi. Mwamtumu Mahiza, alikiri kutokea kwa tukio hilo lakini hakuweza kuthibitisha kama viongozi hao walilazwa chini na kupekuliwa.

1 comment:

  1. KWANI SHEIKH NURUDIN KISHKI NI MTANZANIA KWA KUZALIWA?
    NI SIRI ILIYO WAZI KUWA YEYE NA VIJANA WENGINE WATATU WALIINGIZWA NCHINI TANZANIA NA BWANA MMOJA (MJOMBA WAO) AITWAYE SHATRY WAKITOKEA KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI WA SOMALIA NCHINI KENYA MWANZONI MWA MIAKA YA 90.
    GHARIIB KUN ADIIB.

    ReplyDelete