Friday, November 9, 2012

NASAHA ZATOLEWA KWA KATIBU WA MUFTI,SHK SORAGA, NA KINA-Abdallah BIN Ubbay BIN Saluul !

Baada ya kuwa Katibu wa Mufti Zanzibar amemwagiwa tindikali wakati akifanya mazoezi asubuhi  na hivi sasa amewahishwa hospitali ya Muhimbili kwa matibabu.
Kwa heikh Soraga alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi kwenye viwanja vya Mwanakwerekwe majira ya  asubuhi.
Sheikh Soraga aliwahishwa hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar kwa matibabu ya haraka kabla ya kuamuliwa awahishwe hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

HII NI SEHEMU TU YA NASAHA KWA  SHEKH SORAGA, NA WENZAKE !

""Baada ya kumshukuru Allah nakumtakia rehma bwana Mtume saw ,nataka tuhadharishane juu ya kauli iliyotolewa na mmoja wa masheikh wa hapa zanzibar katika hutba ya Iddi msikiti wa Muembe shauri hotuba ambayo imehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Makamo Wake ,Mabalozi,na Uongozi mzima wa Serikali.Katika hutba hii amezung...

umza kwa ukali juu matokeo yaliyofanyikana juu uharibifu wa Amani,na kuitetea Serikiali kuingia gharama na kulaani jumuiaya uamsho kama ni kikundi kichache kinachotaka kuharibu Amani Zanzibar.

Katika khotuba yake amewataka Wazanzibar kutokubali kusikiza na kutii viongozi wa Jumuiyah ya Uamsho na tuungane wazanzibar kuwapiga vita viongozi kama hawa.huku akisema kwanini Alqaida na Alshabaab walitoka Mogadishu? Akasema raia wenyewe walisema basi tumechoka wakawatowa watu ambao wameisumbuwa Serikali ya Somalia kwa muda mrefu.

Mimi nasema yeye kama mwanachuoni anatakiwa siku zote kufuata haki na si utashi wake mwenyewe ama kwa kujipendekeza ama kwa kutaka sifa ama kwa kunyemelea cheo.Sifa za wanachuoni siku zote lengo lao ni kudhihirisha haki ambayo alitumilizwa nayo Mtume saw ili iwe dini yote ni kwa ajili ya Allah na liwe neno lake Allah liko juu kuliko kitu chengine,na huku wakijuwa ya kuwa kuna mipaka ya kuchunga kuingia kwenye batili,mizozo,na usaliti.Mwanachuoni kama mwanachuoni juu ya ilmu yake na ubora wake hukubali haki vile ilivyo hata kama aliyesema ni mtoto mdogo.Ahli salaf waliopita walikuwa wanawausia jamaa zao na wafuasi wao kuikubali haki inapodhihiri hata kama hawakusema wao.

Sasa sheikh kama huyu kuwafananisha wenzake wanachuoni na Alshabaab na Alqaida huku akitaka serikali na wananchi kuwapiga vita na kutokubali kuwafuata lengo lake nini? Hivyo ndivyo waislamu wanavyotakiwa,kwa mtazamo wa ulimwengu ulivyo sasa hivi kuwafananisha masheikh wakiislamu na makundi hayo nikutumbukiza kwenye shimo la moto jee ndiyo kumfuata Mtume ama ni kumuasi mtume? Na lipi kubwa wanalosema mpaka wafananishwe na Alqaida?

Viongozi wa Uamsho walichofanya na kutaka ni kuwahamasisha wananchi wa Zanzibar kujuwa haki yao ambayo ni kupatikana Dola kamili yenye mamlaka kamili kitaifa na Kimataifa,hapa kuna kosa gani kwa sababu tu wamesema hawataki Muungano?na hili si jipya kudai mtu Dola yake hasa kwa sisi waislamu na wasiokuwa waislamu.shekhe huyu hasomi historia? Wakati Sayyidna Ali alipoihamisha Dola ya Kiislamu Kutoka Madina kuipeleka Iraq mbona Mama Aisha mke wa Mtume saw alikuja juu akiwaita maswahaba wakubwa akina Zubeyri bin Awwaam na Twalha akiwashauri vipi Aliy aichukuwe dola ya kiislam ambayo Mtume saw aliasisi hapa Madina aipeleke Iraq ikawa ni mzozo mpaka ikawa Vita vikaitwa Ghazwatul Jamal na hawa nao ni Alqaida?ama ni Al shabaab kwa kuwa wametaka Dola irudi Madina? Hapa kuna tofauti gani ya kutaka watu wapate Dola yao kamili yenye heshma kitaifa na kimataifa wakati hao hao ndio watofaidika ikipatikana kuliko hawo wanaojadiliwa ni waovu.

Ninachosema mwanachuoni wa kweli akiona haki haipondi na kuikanyaga huwa unaingia katika dalili za kinafiki na usaliti na huo si mwendo sahihi wa mtume wala Maswahaba wala Ahli salaf wema waliotutangulia hebu angalia uadilifu wa waliotutangulia Sayyidina Umar r.a anatangaza watu wapunguze mahari hapo hapo mwanamke kainuka akamwambia Umar unataka kutupokonya haki ambayo m/Mungu ametupa? Mwanamke kama yule aka
soma aya kama hii
وإن أردتم اسنبدال زوج مكان زوج وءاتيتم إحداىهن قنطارا فلا تأخذوا منه شيئا ,أتأخذونه بهتنا وإثما مبينا.
Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya
mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhulma na kosa
lilio wazi?.baada ya kusomewa aya hiyo sayyidna Umar hakuwa makali bali alirudi chini akasema hakika amesibu mwanamke(amepata)na amekosea Ummar.kwanini tusichukuwe mifano hiyo iwe ni kutumia neema ya ufasaha aliyokupa m/Mungu kuwasuta wenzako.hakika kukaa juu ya viriri kuwasengenya na kuwashambulia wanachuoni wenzako hili si jambo zuri Bwana mtume amesema “ENYI MLIOAMINI KWA NDIMI ZENU NA HAMKUAMINI KWA NYOYO ZENU MUSIWAUDHI WAISLAMU,NA WALA MUSIWAFUATIE AIBU ZAO,HAKIKA YEYOTE ATAKAYE WAFUATA KWA AIBU ZAO NA MUNGU NAYE ATAMFUATA KWA AIBU ZAKE,NA MUNGU AKIMFUATA AIBU ZAKE ATAMFEDHEHESHA JAPO KATIKA UPENU WA NYUMBA YAKE”.

Wewe kama Sheikh inakuwaje udhanie wenzako vibaya ya kwamba ndio chanzo cha kuleta vurugu katika nchi na ndio sababu ya uvunjaji wa Amani,uko na uhakika gani juu ya hili kwa kuwa wanataka Zanzibar huru ndio kuvunja Amani kwani Allah si anapenda waja wake wawe huru?Maquraishi vitu walivyo wakililia ni Uhuru na njaa na kila Taifa leo linalia na mambo hayo kwani uhuru ni kujipangia mambo yako bila ya kuingiliwa bila ya woga na leo ndilo linalotakikana kwa Zanzibar leo haiko huru hawewezi kujiamulia mambo yao wako na woga hata makamo wa kwanza wa Rais alithibitisha hilo na kusema sisi tuko na serikali lakini tumenyonyolewa Mbawa.maana yake hawana uhuru wako na uwoga wa kujiamulia kwani kila kitu mpaka waamuliwe.makuraishi walipolilia uhuru na njaa Allah aliwapa sharti moja tu soma suratulfill Allah anasema “Basi nawaabudie bwana wa nyumba hii kaaba ambaye anawalisha kutokana na njaa na akawapa amani kutokana na khofu”.

Wazanzibatr nikimalizia nasema katika dini kuna kitu kinaitwa NASWIIHA(Nasaha) na TAABIIR(ujanja wa nasaha) Sheikh huyu leo siku tukufu baada ya kutumia nasaha inayotakiwa katika dini kipindi kigumu tulichonacho katika nchi kurudisha imani kwa wananchi na serikali yao na viongozi wa dini ndio amekoroga kabisa kuwagawa waislamu hiyo ndio sheria ya dini ikiwa waislamu wamegombana wakatwe mapande ama ni kunasihiana na kuwapatanisha? Maana dini inasema ikiwa makundi mawili ya waislamu yanagombana basi wapatanisheni kundi moja likikataa haki ya kupatanishwa lipigwe vita mpaka lirudi kwa M/Mungu sasa nauliza katika wazanzibar wanaotaka Dola yao kamili na wale wanaopinga wapi wana makosa?

Cha kutahadharisha ni kuwa khutba ile si ya nasaha kwa waislamu bali ni TAABIRI yaani kujifanya unazungumzia kitu kwa nasaha ili uonekane unasema mazuri na kuelekeza kwenye haki lengo likawa ni kinyume kabisa kumbe wajifanya kutetea haki bali ni kuitangaza batili hatusemi tunaunga mkono watu wafanye fujo,wamwage damu,wafunjiane heshima,kuporana mali, hapana lakini isiwe sababu ya kutuona ukweli wa kile kinachodaiwa.

Na unafiki namna hii ulikuweko hata kwa baadhi ya maswahaba kujidai wanafanya jambo zuri kumbe ni kinyume ni fitina tupu mfano Abdallah BIN Ubbay BIN Saluul alijenga msikiti nzuri na kuupamba huku akimtaka mtume aache msikiti wake aende kule,Allah akamkataza akamwambia msikiti uliojengwa kwa misingi ya ucha mungu ni bora kuliko ule uliojengwa kwa ria na kutaka kuwagawa waislamu.maana yake nini?ukiangalia kwa mtazamo wa nje msikiti ni nyumba ya mungu lakini kumbe sifa za msikiti hauna vile inavyotakikana,na ndio nikasema khutba ya leo utaona ni khutba ya kutaka tuwe wamoja kumbe ni kinyume maana yake tufarikiane.ndio nikasema si NASWAAHA BALI NI TAABIIR.
""

No comments:

Post a Comment