Mwanafunzi toka Kenya mwenye umri wa miaka 21 anashikiliwa na polisi nchini Kenya baada ya kumuua mwanafunzi mwenzake toka Ghana na kisha kuula moyo wake na sehemu ya ubongo wake.
Alexander Kinyua mwanafunzi toka Kenya aliyekuwa akiishi nchini Marekani akisoma kozi ya uhandisi umeme katika chuo Morgan State University alimuua mwanafunzi mwenzake aliyekuwa akiishi naye nyumba moja, Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie ambaye ni mwanafunzi toka Ghana mwenye umri wa miaka 37.
Kinyua alimuua Kujoe na kisha kuikata miguu yake na mikono yake kabla ya kuunyofoa na kuula moyo wake na sehemu za ubongo wake.
Vipande vya mwili wa Kujoe vilipatikana wiki moja baada ya taarifa za kupotea na kutoonekana kwa Kujoe kupelekwa polisi.
Polisi wa Marekani walitoa taarifa iliyosema kuwa Kinyua amekiri kumuua Kujoe na kula baadhi ya viungo vya mwili wake. Taarifa hiyo ya polisi ilisema kuwa Kinyua alisema kuwa alimuua Kujoe na kisha kukikata kichwa chake na mikono yake na kuihifadhi kwenye nyumba wanayoishi wazazi wake kwenye kitongoji cha Joppatowne.
Taarifa zilizopatikana baadae toka kwa marafiki zake zilisema kuwa Kinyua ambaye alikuwa tayari ameishapewa uraia wa Marekani alikuwa akionyesha dalili kuwa ana stress sana na yupo kwenye depression.

No comments:
Post a Comment