Friday, March 22, 2013

bilal waikera na shekh ponda walivyotoa ushahidi wao mahakamani majuzi

MZEE Bilal Waikela (mwenye bakora) akitoka nje ya mahakama ya
Kisutu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada
ya kutoa ushahidi wake katika kesi ya Sheikh Ponda.

MZEE Bilali Rehan Waikela(87), ameiambia Mahakamaya Hakim Mkazi Kisutu,Jijini Dar es Salaam kuwa,kuuzwa ardhi ya Waqfu,Markazi Chang’ombe niaibu na dhulma kubwa dhidi ya Waislamu nchini.

Mzee Waikela, amesemahayo Jumatano wiki hii mbele ya Hakim Mkazi waMahakama hiyo Bi. Victoria Nongwa, wakati akitoaushahidi wake katika kesiya jinai namba 245/2012,inayomkabili Sheikh PondaIssa Ponda na wenzake.Akiongozwa na mawakiliwa upande wa utetezi Bw.Juma Nassoro na Yahya Njama, Mzee Waikelaaliiomba Mahakama hiyokuirudisha ardhi hiyo kwaWaislamu, kwani BAKWATAwamefanya dhambi kubwakwa hatua yao ya kuiuza hukuwakijua mali ya waqfu nainahitaji kufanyiwa uadilifu.“Naiambia Mahakamakuwa aibu iliyofanyikani kubwa kwa mujibu waDini yetu, labda wapaganindiyo wanaweza kufanyahivyo. Naiambia Mahakamawairudishe ardhi hiyo kwaWaislamu, kwani hatuawaliyoichukuwa si sahihi.”Alisema Mzee Waikela.Mzee Waikela ambayeni mmoja wa waasisi waChama cha siasa cha TAA,kisha TANU, na kiongoziwa iliyokuwa Jumuiya yaWaislamu ya Afrika Mashariki(EAMWS), aliiambiaMahakama kuwa mali yaWaqfu kamwe haiwezi kuuzwahata kama imerithiwa.Akielezea ufahamu wake juu ya kiwanja cha MarkaziChang’ombe, Mzee Waikelaambaye alikuwa ni Katibu waEast Africa muslim WalfareSociety (EAMWS) mkoawa Tabora, alisema kiwanjahicho kilipatikana kipindi chauongozi wa Jumuiya hiyo yaWaislamu, chini ya uongoziwa Agakhan na Rais wa Misriwakati huo Gamar Abdul Nasser.Alisema kupitia Jumuiyahiyo, zilifanyika juhudikupata kiwanja hicho lengona madhumuni likiwa nikujengwa Chuo Kikuu ChaWaislamu kwa awamu tatu,kwa msaada wa Rais wa Misriwa wakati huo Gamar Abdul Nasser.Alipoulizwa ni kitu ganikilikwamisha adhima hiyo,Mzee Waikela aliwatajaaliowaita ‘mafatani’wakishirikiana na watu


wabaya, ambao walipangamikakati ya kuiuwa EAMWSna kuwaundia WaislamuBAKWATA.Alisema njama za kuiuwaEAMWS, zilifanywa naMwalimu Nyerere akimtumiaMzee Abeid Karume, kwakuwalaghai Waislamu ambaoaliwataja baadhi yao kuwa niAdam Nassib, Saleh Masasina Qassim Bin Jumaa.Mzee Waikela alisema, watuhao walizunguka katika mikoaishirini nchini wakati huona kuwashawishi Waislamukuikataa na kutengana naEAMWS. Hata hivyo alidaifitna yao ilifanikiwa katikamikoa nane na mikoa 12waliwakatalia.“Mimi binafsi nilikuwampinzani wa kuitenga nakuiuwa EAMWS, katiya mwaka 1968/9, kwaniwalifika akina Adam Nasibuna watu wake na kunishawishikwa kunipa Shilingi 40/=,nilizikataa wakaondoka.”Alisema Mzee Waikela.Alisema baada ya juhudihizo za kuwalazimishaWaislamu kuikataa Jumuiyayao, ilitumika Serikalikupitia Waziri wa Mambo ya Ndani wakati huo,
 Bw. SaidiMasanywa, kwa kusimamiakufungwa ofisi zote na malizote za Jumuiya zilizokuwanchi nzima kukabidhiwaBakwata.Aliongeza kuwa katikakuonyesha kwake upinzanikatika kuiuwa EAMWS,alijikuta kati ya mwaka 1963na 1964, akiwekwa kizuizina Mwalimu Julius Nyerere,wakati huo akiwa Rais waJamhuri ya Muungano.“Naiambia Mahakanakwamba, kiwanja chaMarkaz si mali ya Bakwata,wakati tunapewa kiwanjahicho Bakwata haipo,imekuja baadae kwa hilana inda pasi ya ridhaa yaWaislamu na kuhodhi maliza waislamu zikiwemo zaWaqfu.” Alisema Mzee Bilali, baada ya kuulizwa na wakili Nassoro kuwa anaiambia niniMahakama kuhusu madai yaumiliki wa Bakwata katikaeneo hilo.Aidha alifafanua kuwa waokama Jumuiya ya Waislamu,walisimamia mali za Waislamukikiwemo kiwanja hicho kwaajili ya maendeleo yao, lakinialidai baada ya mali hizokuhodhiwa na Serikali nakuikabidhi Bakwata, malinyingi za Waislamu zimeuzwakwa bei chee, si Dar es Salaamtu bali hata zile zilizokokatika mikoa mingine na malinyingine walikimilikisha watuwa Bakwata.“Mfano wa karibu ni hichokiwanja cha Chang’ombe,tulikabidhiwa likuwa nieneo kubwa sana tofauti nasasa, nasikia kimemegwa nakuuziwa watu. Lakini iwemtu kapewa ama kauziwa,aelewe kabisa kuwa mbeleya Mwenyezi Mungu si maliyake, ni mali ya Waislamu,mali ya waqfu haiuzwi,hagaiwi mtu.” Alisema MzeeWaikela.

Akijibu maswali ya wakiliwa Serikali Bw. TumainiKweka, Mzee Waikela alisemaBakwata haipo kwa haki,ukifuatwa msingi wa kuundachombo kwa kuzingatiademokrasia, kwani katika juhudi za Bw. Nassibu nakundi lake mikoani, ni mikoanane tu ndio iliunga mkonokuvunjwa kwa EAMWS katiya mikoa 20.Alipoulizwa kamaanaikubali Bakwata, alisemahaikubali, si sasa tu bali aliikataa tangu kuanza kwamchakato wake na baadaya kuundwa kwawe mkoaniIringa na mpaka sasa badohaikubali.“Mimi Bakwata siitambui,niliikata tokea wakati huochini ya Sawaya (Waziri waMambo ya Ndani wakatihuo), nikawekwa kizuizinina Nyerere, Bakwata imemilikishwa mali zaWaislamu kinguvu, kimsingimali hizo si za Bakwata ni zaWaislamu.” Alisema MzeeWaikela, ambaye pia alikuwakiongozi wa Baraza la MisikitiTanganyika.

Akijibu hoja ya wakiliwa serikali Tumaini Kweka,kuwa waliounda Bakwatamkoani Iringa walikuwani Waislamu, Mzee Bilali alisema wale walikuwa niviongozi wa matawi ya Chama,na hawakuwawakilishaWaislamu kwani alidai halihalisi ilishaonyesha kuwakati ya mikoa 20 ni mikoanane tu iliyokubali. Alisisitizakwamba shughuli za dinihaziendeshwi na viongoziwa siasa bali ni viongozi wadini.Ama alipoelezwa kuwahakuikubali Bakwata kwakuwa alikosa donge, alisemawakati huo hakuwa na dhikiya pesa bali alikuwa ni mtumwenye mali zake na hatawakati anaingia katika siasa pia hakuwa na dhiki.“Sikuikataa Bakwata kwachuki, mimi nilikuwa na pesazangu hata wakati napambanana kupata Uhuru, nilikuwanatoa motokaa (gari) yangukwa Nyerere (Rais) akijaTabora atumie, lengo lilikuwani Waislamu kutendewa haki,nimeikataa kwa sababu yakupindishwa haki.” AlisemaMzee huyo.Kwa ujumla Mzee Waikela,aliianishia Mahakama yaHakim Mkazi Kisutu kwamba, Waislamu nchini wanatenzwanguvu ndani ya Bakwata,kwani alidai kuwa iwapoikitokea Waislamu kupigakura kama wanaikubaliau hawaitaki Bakwata,itaanguka

.Hata hivyo Mzee Waikela,alisema hadhani kamainaweza kutokea fursa hiyokwa Waislamu kwani anajuakuwa maslahi ya walioundachombo hicho yataharibika.Katika hatua nyingine kwamara ya kwanza, jana SheikhPonda Issa Ponda, alisimamakatika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mbele yaHakimu Mkazi wa Mahakamahiyo Victoria Nongwa nakutoa ushahidi wake.Akianza kutoa ushahidiMahakani hapo, SheikhPonda alisema kuwa, ni kwelikiwanja hicho kina mgogoro,ambapo Waislamu wanapingaeneo lao kupewa kampuniya Agritanza, ambayo inadaikumiliki kiwanja hicho kwakubadilishana na Bakwata,ambao nao walipewa kiwanjakingine huko Kisarawe.Sheikh Ponda, alisemamigogoro ya viwanja eneola Markaz Chang’ombe ni yamuda mrefu, ambapo kunawakati sehemu nyingineya eneo hilo la MarkazChang’ombe, lilimegwa nakuuziwa mfanyabiasharamaarufu Yusuf Manji, kinyumena matakwa ya Waislamuambao ndio wenye mali.Alisema katika sakata hiloWaislamu walipinga ambapo baadhi yao walikwendaMahakamani, na wenginekwenda Serikalini kupingakuuzwa eneo hilo.Alisema eneo hilo laMarkaz awali lilikuwa kubwa,lakini sasa limebaki dogosana kutokana na tabia yakumegwa kinyemela bilaWaislamu kujulishwa.Kuhusu kiwanja chenyemzozo kwa sasa, ambachomfanyabiashara Hafidh,anayemiliki Kampuni yaAgritanza inayodai kumilikikiwanja hicho,

 Sheikh Ponda aliieleza Mahakama kuwamara baada ya kupata taarifaza eneo hilo la Markazkumegwa tena, walimfuatiliamtu aliyedaiwa kulimega ilikujua kulikoni.Sheikh Ponda alisemaWaislamu kupitia baadhi yaMasheikh, akiwemo yeye naSheikh Lwambo, walikutanana Hafidh ambapo walipangasiku ya kukutana kujadilitatizo hilo.Alisema baada ya kukutana,walimweleza Bw. Hafidh kuwakiwanja anachodai kupewa niwaqfu, kwa maana kuwa nimali ya Waislam ambayo hairuhusiwi mtu kuuza,kuuziwa wala kujimilikisha isipokuwa ni kwa ajili yamatumizi ya dini, kwa maanaya matumizi ya masuala yaWaislamu.Akiendelea kutoa ushahidiwake Sheikh Ponda alisema kufuatia kikao hicho,walikubaliana na Bw. Hafidh kuwa asitishe kujihusisha nakiwanja hicho na kwamba,atatafutiwa kiwanja kingine.Sheikh Ponda, aliwasilisha muhtasari wa kikao kati yaona Bw. Hafidh Mahakamanihapo, waliyokubaliana kuwaBw. Hafidh, hatojihusisha nakiwanja hicho cha Markazkama walivyokubaliana.Hata hivyo,

Sheikh Pondaaliieleza Mahakama kuwa, baada ya makubaliano kufanyika kupitia kikaowalichokaa, walishangaa kuona Bw. Hafidh, akipeleka vifaa katika kiwanja hichona kuanza ujenzi tofauti nawalivyokubaliana.Alisema, baada ya kuona hivyo, walimtafuta Bw.Hafidh na kumuuliza kulikoni akiuke makubaliano ya kikaochao cha awali, ya kukiachakiwanja hicho cha Waislamuna kukubaliana kutafutiwakingine.Alisema, kufuatia haliiliyojitokeza Waislamuwalikubaliana na kuamuakujenga Msikiti wa mudakatika eneo hilo, ili kuhakikishakwamba eneo hilo, haliingiliwina mtu mwingine.Hata hivyo, Sheikh Ponda,alisema siku ya Ijumaa yaOktoba 12, 2012 Waislamuwalipokuwa wakijengaMsikiti wa muda, Bw. Hafidhaliamua kulipeleka suala hilo polisi. Ndipo baadae alisemaSheikh Ponda,

 kwambawalifika Polisi na kuwavamiaWaislamu na kuwasweka ndani.Aidha Sheikh Ponda, aliitakaBakwata kurejesha eneo lotela Waislamu Chang’ombe,kama walivyolikuta wakatilikiwa chini ya East Africa Muslim Walfare Society.Alisema, kitendo chaBwakata kukiri kuwa eneo limebaki dogo lakini lilikuwakubwa, ni wazi kwambakwa njia moja au nyingine kuna watu wameuziwa hukuwakijua kuwa ni eneo lawaqfu.Hivyo Sheikh Ponda,alihitimisha ushahidi wakekwa kuitaka Bakwata kwahali yoyote, kurejesha eneolote la Waislamu.Kesi hiyo imeahirishwa,ambapo April 4, Wakiliupande wa utetezi atawasilishaMahakamani majumuisho yaushahidi uliotolewa ambapo Aprili 18 mwaka huu, kesiitatajwa Mahakamani hapokwa ajili ya hukumu.

No comments:

Post a Comment