Friday, March 22, 2013

itiqaf kubwa kufanyika msikiti wa tungi pekee.yanayowasibu waislamukujadiliwa usiku kuchwa.


WAISLAMU Jijini Dares Salaam, wametakiwakuhudhuria kwa wingikatika ibada ya Itiqaaf,itakayo fanyika katikaMsikiti wa Tungi, Temeke.
Wito huo umetolewa naImam wa Msikiti huo, SheikhShaaban Ibrahim, wakatiakiongea na mwandishi wahabari hizi mapema wiki hii.Alisema kwamba ibadahiyo ni katika mwendelezowa maazimio ya Jumuiyana Taasisi za Kiislamu nayanafanyiwa kazi na Shuraya Maimam, ambapo katikakikao chao Jumapili wikiiliyopita, taarifa za maazimiohayo zilitakiwa kufikisha kwaWaislamu kupitia Misikitiyao.Sheikh Ibrahim, alisemalengo la Itiqafu hizo ni kumliliana kumkabidhi MwenyeziMungu kile kinachoonekanakuwa ni dhulma dhidi yaWaislamu, kupuuzwa nakunyimwa haki zao.

Alifafanua Sheikh huyokwamba, kabla ya kuanzakwa ibada hiyo ya Itiqaaf,Waislamu wapewe dakikamoja hadi mbili kunuia nakukabidhi kwa MwenyeziMungu wale ambao ni kikwazokatika harakati zao.Aidha alisema kuwa,viongozi wa Waislamuwatapata fursa ya kuongea naWaislamu kuwaeleza mamboyanavyoendelea kuhusukadhia mbalimbali dhidi yaona namna gani wanakabiliananayo.Taarifa zaidi kutoka Shuraya Maimam zimeeleza kuwawakati hayo yakifanyika,viongozi wa Kiislamu wanajipanga kwa hatuambadala katika kudaikutekelezewa madai yaoSerikalini.Hii inakuwa ni Ibadaya pili ya Itiqaf, kufanyika baada ya kutanguliwa na ileiliyoswaliwa katika Msikiti waKichangani (T.I.C) Magomeni,Jijini Dar es Salaam Jumamosiwiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment