wengine waliburuzwa hivi. |
Washitakiwa 52 kati ya 54 katika kesi ya kula njama na kufanya maandamano isivyo halali wamehukumiwa kwenda jela kila mmoja baada ya kukutwa na makosa matatu huku mmoja akiachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia na mwingine kufariki dunia kabla ya hukumu iliyotolewa leo na hakimu Sundi Fimbo wa Mahakama ya Hamimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao walidaiwa kutenda kosa Februari 15 mwaka huu.
Baada ya pande zote kusikilizwa na washtakiwa kutoa hoja za utetezi, hatimaye hakimu Fimbo alitoa hukumu hiyo leo ambapo aliwatia hatiani washtakiwa 52 kwa makosa matatu kati ya manne na kila mmoja akamhukumu kwenda jela mwaka mmoja kwa kila kosa.
Hata hivyo, Fimbo akasema washtakiwa hao watakwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa vile adhabu zote zinakwenda kwa pamoja.
askari waliwahukumu kurukakichura kabla hata ya kufungua jalada la kesi yao. hapani mara tu baada ya kukamatwa waliamriwa kuruka kichurachura wakiingizwa makao makuu ya jeshi la polisi la tanzania. |
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo leo, wakili Mohamed Tibanyendera alimtaka hakimu awapunguzie adhabu wateja wake kwavile wengi wao wanategemewa na familia zao na kwamba, tayari walishakaa mahabusu kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.
Washitakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Salum Makame, Said Idd na Ally Nandumbi, Makame, Idd na Nandumbi, Hussein Athumani, Seif Rwambo, Abdull Ally, Waziri Swed, Naziru Waziri, Ahmad Rashid, Jumanne Kayogola, Hamis Tita, Amri Diyaga, Salum Said, Rajabu Mpita na Haji Sheluhenda, Abdul Ahmed, Bakari Mwambele, Ramadhani Fadhili, Awadh Juma, Omari Mkwau, Kassim Chobo, Abubakari Bakari, Ramadhani Milambo, Hamis Ndeka, Athuman Juma, Abdallah Salum, Juma Makoti, Bashir Kakatu, Imam Omari, Rashid Lukuta na Bakari Athumani, Mbwana Kassim, Nurdin Ahmed, Mustapha Mide, Rajabu Kifumbo, Zuberi Juma, Omari Mkandi, Idrisa Katulimo, Sawali Mola, Said Dudu, Ramadhani Juma, Musa Sinde, Issa Sobo, Yahaya Salum, Jabil Twahil, Shomari Tarimo, Hashim Bendera, Waziri Toy, Athuman Yahaya, Yasin Seleman, Shaban Malenda, Yasin Mohamed, Khatib Abdallah na Rajabu Rashid wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
waliokuwa baadhi ya viongozi wa waislamu. |
Shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kusababisha uvunjifu wa amani.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola, alidai katika shitaka la tatu kuwa siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, washtakiwa wote kwa pamoja baada ya Jeshi la Polisi kutoa zuio la kufanya maandamano, walikiuka amri hiyo na kufanya mkusanyiko ulisababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
Katika shitaka la nne, ilidaiwa kuwa mshtakiwa Makame, Idd na Nandumbi, waliwashawishi wananchi kwa kuwasambazia vipeperushi vya kuhamasisha kufanya maandamano yasiyo halali.
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, vilio vilitawala katika viunga vya mahakama vilivyofurika watu kufuatia baadhi ya ndugu na jamaa wa washtakiwa kuangua kilio, wasiamini kile kinachotokea.
Baadaye washtakiwa walipandishwa kwenye karandinga na kupelekwa gerezani.
No comments:
Post a Comment