akiwataka wakae mbali na 'magaidi' hao. Kutokana na chuki iliyojengeka shuleni hapo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani
ameamua kufunga shule hiyo huku hatma ya Mkuu huyo wa Shule ya Sekondari ya Bagamoyo, Bw. Bonus Ndimbo,
akiiacha mikononi mwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Hajjat Mwantum Mahiza, amelazimika kufunga Shule hiyo mapema wiki hii, baada ya kuwepo
mgogoro wa Kidini Shuleni hapo kwa muda mrefu jambo linaloashiria hali ya hatari. Akiongea na mwandishi wa habari
hizi, Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani, baada ya kutangaza kuifunga Shule hiyo, alisema suala hilo amelikabidhi kwa
Wizara husika (Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi) kwa ajili ya uchunguzi zaidi juu ya mgogoro huo na hatma yake.
Hajjat Mahiza, alisema jukum lake akiwa kama Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa, ni kuhakikisha usalama ndio
maana alimechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuna matatizo katika uongozi na wanafunzi shuleni hapo. Alisema,
baada ya kufika Shuleni hapo, alibaini kuna tatizo la kiutawala kwa walimu na tatizo la nidhamu kwa wanafunzi, kwani
alidai wanafunzi wengi hawakuwapo Shuleni huku uongozi wa shule haujui wanafunzi hao wapo wapi. An nuur, ilipotaka
kujua uhalali wa barua ambazo walipewa wanafunzi tisa wa Kiislamu wa Shule hiyo na Bodi ya Shule kwa lengo
kuwasimamisha Shule kisha wanafunzi hao kugoma kuzipokea na kusaini, alisema hilo ni miongoni mwa mambo ambayo
Wizara itashughulika nalo katika uchunguzi wake na wanaotakiwa kuzitolea ufafanuzi ni Wizara husika.
" M i m i s i o Wi z a r a y a Elimu, zile barua zitafanyiwa kazi na Wizara ya Elimu, wao ndio wataeleza hiyo adhabu
iliyotolewa na Bodi ni sahihi au la baada ya kujua chimbuko la mgogoro huo." Alisema. Kufuatia kufungwa kwa Shule
hiyo, tokea jumanne wiki hii, wanafunzi wamekuwa wakiondoka kwa utaratibu maalum kurejea makwao mpaka hapo
watakapotakiwa kurejea tena shuleni hapo. Kufuatia mgogoro huo wa muda mrefu Shuleni hapo baina ya Wanafuzi wa
Kiislamu na Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Bonus Ndimbo, hali ilikuwa mbaya zaidi Jumatatu wiki hii, pale ambapo Bodi ya
Shule, ilipoamua kuwapa barua za kuwataka wanafunzi tisa wa Kiislamu kuondoka Shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wameeleza kuwa, barua hizo zilikuwa ni za kuwasimamisha wanafunzi hao ambao miongoni mwao
ni viongozi wa Waislamu Shuleni hapo, mpaka Novemba 26, mwaka huu, huku wakidai barua hizo hazikueleza sababu
za msingi wao kusimamishwa. Taarifa zaidi zinasema, wanafunzi hao walipokuwa wakikabidhiwa barua hizo kisha
kutakiwa kusaini, waligoma wakidai bado walikuwa wakisubiri majibu yao ya msingi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya
(Bagamoyo), Bw. Ahmed Kipozi, aliyefika Shuleni hapo siku chachache nyuma na kupokea malalamiko yao na kuahidi
kuwapa majibu ya kero zao dhidi ya Mkuu wa Shule hiyo. Wanafunzi wa Kiislamu Shuleni hapo, baada ya kubaini kuwa
wenzao walikuwa wanatakiwa kusimamishwa Shule, walikusanyana na kufika pale walipo wenzao mbele ya Bodi,
wakitaka barua hizo za kusimamishwa wapewe wote huku wakidai tatizo ni la wanafunzi wote wa Kiislamu. Baada ya
muda, viongozi wa Mkoa na Wilaya, chini ya Mkuu wa Mkoa, Hajjat. Mwantum Mahiza, walifika Shuleni hapo, kisha
kufanya kikao maalum baina ya uongozi na wanafuzi wa Shule, ambayo katika jumla ya mambo aliyoongea Hajjat.
Mahiza, ni kusisitiza umoja na kuvumiliana. Hajjat Mahiza, alinukuliwa akisema, kama mtu anaswali swala tano na
mwingine hawali swala hizo, ni vyema wakavumiliana kwani kila mmoja ndivyo imani yake inaruhusu hivyo. Baada ya
nasaha zake, Mkuu huyo wa Mkoa aliamuru Shule hiyo ifungwe, ili kupisha uchunguzi ufanyike kubaini kiini cha mgogoro
huo kisha hatua stahiki zichukuliwe. Awali, wakielezea chimbuko na chanzo cha mgogoro huo, baadhi ya wanafunzi wa
Shule hiyo (majina tunayahifadhi) kabla na baada ya tukio la kufungwa kwa Shule hiyo, walisema tatizo ni Mkuu wa
Shule, Bw. Bonus Ndimbo, kudhihirisha udini na chuki kutokana na kauli zake kwa wanafunzi wa Kiislamu shuleni hapo.
Walisema, Mwalimu huyo tokea ahamie shuleni hapo amekuwa akitoa kauli za kupandikiza chuki miongoni mwa
wanafunzi wa Kiislamu kwa wenzao wa Wakristo, kwa kuwaita Al-kaida, Alshabab, huku mara kwa mara
akiwatahadharisha Wakristo kuwa mbali na Waislamu. Wanafunzia hao walieleza kuwa mwanafunzi yoyote wa Kiislamu
anayeonekana kuwa anafuata maadili ya dini yake, mwalimu huyo hujenga chuki naye na kumuita Alshabab, huku
akidai kuwa atahakikisha anawapunguza Shuleni hapo. Wanafunzi hao wanamtaja mwanafunzi El-Hakim Somji, aliye na
asili ya Kihindi, kuwa miongoni mwa wanafunzi wanaoandamwa sana na Mkuu wa Shule, akimkejeli kuwa ni Al Shabab.
"Sikupendi na sitokupenda." Wanafunzi hao walimnukuu Mkuu wao, wakidai ni maneno aliyomwambia mwenzao Somji,
huku akimshutumu kuwa ana uhusiano na Alkaida. Walisema, katika kujitete mwanafunzi Somji, ambaye pia ni Katibu
wa wanafunzi wa Shule hiyo na mweka hazina kwa upande wa wanafunzi wa Kiislamu, aliwahi kumueleza Mkuu wake
wa Shule kuwa, anaona hamtendei haki kumuita gaidi wa Al Qaida. Wanafunzi hao walibanisha kwamba, hali
ilijiridhirisha zaidi, kipindi cha uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi kilipofika ambapo Mkuu huyo, alibadili mfumo uliokuwa
ukitumiwa miaka yote shuleni hapo, kwa kila nafasi inayogombewa ilikuwa na watu watatu, lakini kwa utaratibu mpya
kila nafasi alitaka iwe na wagombea wawili, tena Mkristo na Muislamu. Walisema, siku moja kabla ya uchaguzi, Oktoba
3, mwaka huu kupitia katika sanduku la maoni Mkuu wa Shule aliwataja wanafunzi Ramadhani Bilali, na Kaiza
Ruttakinikwa kidato cha Sita CBG, kuwa wanafunzi hao wanashawishi udini Shuleni hapo. Siku ya uchaguzi, (Oktaba
42012), majira ya asubuhi, Mkuu huyo inadaiwa alikwenda na karatazi hiyo ya maoni katika darsa la wanafunzi hao
kisha kuisoma na kabla ya kuisoma alimtaka Ramadhani Bilali, akamsubiri ofisini kwake. Inadaiwa kuwa, akiwa darasani,
Mkuu huyo anadaiwa kusema kuwa kuna watu wanajifanya kujua sana dini Shuleni hapo, huku akiwashawishi
wanafunzi kutowasikiliza na kuwapuuza kama watu wa sokoni. "Kuna watu hawapaswi kufuatwa, mfano kama hawa
wanaoswali swali sana, kutwa nzima wanaswali tu. Mwenyezi Mungu ameweka siku moja tu ya kuswali." Kilisema
chanzo chetu, kikimnukuu Mkuu huyo. Imeelezwa kuwa akitoa lawama hizo darasani, mwanafunzi aliyetajwa kwa jina la
Japhet Kazimili (Mkristo) alipingana na Mkuu huyo, akisema kuwa huenda taarifa hizo amezipata tofauti kwani alidai,
hakuna udini kama anavyodai (Mkuu). Chanzo chetu kilisema, Mkuu huyo alimtuhumu mwanafunzi Ramadhani Bilali
ambaye ni kiongozi wa wanafunzi wa Kiislamu kuwa ni Alshabab na ni mdini na kuwa hayupo peke yake Shuleni hapo.
Siku hiyo ya Oktaba, 4, 2012, ambayo ndiyo ilikuwa siku ya uchaguzi wa wanafunzi, wakiwa mstarini Mkuu wa Shule,
aliisoma ile barua ya maoni kisha alitoa orodha ya wanafunzi Ramadhani Bilali (Kiongozi wa Da'awa na taaluma kwa
Waislamu), Kaiza Ruttakinikwa, El-Hakim Somji, Answaar Abdulhakim, Amin Thabit (Amir wa Jumuiya ya wanafunzi wa
Kiislamu), akisema anawatahadharisha na watu hao sana Shuleni hapo, kisha aliakhirisha uchaguzi huo na kusema
utafanyika siku inayofuata, Oktoba 5, 2012. Kufuatia kauli hizo za Mkuu wa Shule, wanafunzi Waislamu waliokuwa
wakigombea katika nafasi mbalimbali waliandika barua za kujitoa katika uchaguzi, kwani miongoni mwa waliotajwa siku
hiyo miongoni mwao ni wagombea, hivyo walidai Mkuu alidhamilia kuvuruga uchaguzi kwa kuwatangazia sifa mbaya
mbele ya wapiga kura (wanafunzi). Hata hivyo uchaguzi huo uliendelea siku hiyo huku wanafuzni wa Kikristo
wakinukuliwa wakitamba kuwa wanaenda 'kusimika Kanisa', huku Mkuu akisema, kujitoa kwa wagombea hao wametumia
demokrasia yao hivyo hawezi kuahirisha uchaguzi hukuakionyesha kuridhishwa na hali hiyo. " Tu l i a n d i k a b a r u a
k w a Mkuu kuonyesha kuchoshwa na mwenendo wake mzima na kwamba anapandikiza mbegu za udini na
kutengeneza matabaka miongoni mwa wanafunzi shuleni hapo ambao kabla ya ujio wake matatizo hayo hayakuwepo."
Alisema mwanafunzi mmoja. Oktoba 15, mwaka huu, waliamua kuelekea kwa Mkuu wa Wilaya kupeleka malalamiko yao,
hata hivyo njiani walikutana na Jeshi la Polisi, na kuwazuia na walipoulizwa walieleza nia yao ya kumuona Mkuu. "Polisi
walituomba turudi na kutuitia Afisa Elimu wa Wilaya (D.E.O), Mwl. Majoyo, ambaye tuliamini ni mtu ambaye atatusaidia
kutatua matatizo yetu na Mkuu wa Shule, baada ya kutusikiliza alihaidi kulifanyia kazi na kututaka kurudi madarasani ili
amsikilize na Mkuu pia kabla ya kutoa majibu ya pamoja." Alisema
No comments:
Post a Comment