LECTURE BUILIDING NI HII |
Pinda alisema fedha hizo zitakopeshwa kwa wanafunzi wanaosoma masomo hayo katika vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Alisema serikali inatambua mchango mkubwa ambao umekuwa ukitolewa na vyuo binafsi, na kuongeza kwamba hadi sasa kuna vyuo vikuu 33 vinavyofundisha masomo ya sayansi, na kati ya hivyo 21 ni vya binafsi huku vya serikali vikiwa 12.
Aliwasihi viongozi na wazazi kutowakataza watoto wao kusoma masomo hayo kisa tu wao huko nyuma hawakusoma.
Hata hivyo, alitaka vyuo binafsi kuhakikisha vinaangalia namna ya kutoa fursa kwa watoto wa masikini, ambao wamejikuta wakishindwa kupata elimu hiyo kutokana na kukosa fedha.
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Dk. Arul Raj, aliwataka wanafunzi waliohitimu kuhakikisha wanairudishia jamii na wazazi kile walichokisoma kwa muda wote chuoni hapo.
WAHINDI NDO MPANGO MZIMA HAPA ! |
NDANI YA ELECTRONIC LAB MAMBO YAKE NI DIGITAL. |
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, aliyemwakilisha Askofu Mkuu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, alisema kanisa lao litaendelea kujenga vyuo vyenye kutoa elimu ya sayansi, ili kuweza kusaidia nchi kufikia malengo ya milenia katika kuwapa watu wake elimu na kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani.
No comments:
Post a Comment