Kufuatia mabomu yaliyopigwa mwishoni mwa mbio ndefu katika mji wa Boston nchini Marekani ambaye
Erik Rush. |
Erik Rush ambaye ni mchambuzi wa habari ambaye hualikwa kwenye televisheni ya Fox News ya Marekani amesababisha mtafaruku kwa kuandika kwenye twiter yake kuwa Waislamu ni waovu na inabidi wauliwe.
Rush alikuwa akiongelea milipuko miwili ambayo ilitokea mjini Boston karibu na mstari wa kumalizia mbio ndefu ambapo watu watatu walifariki huku watu wengi wakijeruhiwa na wengine wakiwa wamekatika miguu.
Wakati hadi sasa hakuna taarifa zilizotolewa juu ya watu waliofanya shambulizi hilo, Rush alienda moja kwa moja na kudai kuwa aliyefanya shambulizi hilo anatoka nchini Saudi Arabia.
Alipojibiwa twiter yake kama anawalaumu waislamu kwa kuwahusisha na milipuko ya mabomu huko Boston, Rush alijibu kwa kusema "Ndio, Waislamu ni Waovu, Tuwaueni wote".
Rush ambaye mwaka 2009 aliwahi kutoa makala aliyoipa jina la "Yes Islam is an Enemy" amekuwa mchambuzi wa habari kwenye televisheni ya Fox News na alijipatia umaarufu wakati wa uchambuzi wa uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 2008.
Kauli yake hii ya kuhimiza kuuliwa kwa waislamu imepokelewa kwa hasira na watu wengi waislamu na wale ambao si waislamu.
Mmoja wa wakazi wa Boston alijibu twiter hiyo kwa kusema "Kuna mtu Fox News ameandika kwenye twiter "Waueni Waislamu Wote" baada ya milipuko. Nikiwa kama mkazi wa Boston na kama binadamu nimesikitishwa sana".
No comments:
Post a Comment