walikutana katika ukumbi wa serena hotel leo. |
Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama inayojumuisha Askari wa Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa pamoja Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) imelazimika kukutana na viongozi wa dini kwa lengo la kujadili masuala ya usalama wa nchi, kikao hicho kilichofanyika, jijini Dar es Salaam kimeshirikisha viongozi 300 wa dini kutoka pande zote mbili.
Taarifa za ndani zilizonaswa na kaachonjo blog kutoka ndani ya Kikao hicho zinadai kwamba, mambo ya msingi yanaendelea kujadiliwa ni nafasi ya viongozi wa dini katika Ulinzi na Usalama wa nchi.
"Mimi niko nje ya hicho kikao ila Kamanda yuko kwenye hicho kikao tangu asubuhi, ingawa sina hakika na ajenda za kikao hicho, lakini ajenda kubwa ninayoifahamu ni kwamba viongozi hao wa dini wanajadili ajenda ya usalama"alisema mmoja wa wasaidizi wa Kamanda mmoja wa Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo uliofunguliwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, ulijumuisha viongozi wa dini 150 kutoka kila upande,ambapo aliwataka watambue kuwa mustakabali wa nchi uko chini yao kwa sababu wao ndiyo wanaokutana waumini wa dini hizo kila wakati.
Katika tukio hilo watu wawili walifariki dunia na wengine 62 kujeruhiwa vibaya, waliofariki dunia nipamoja na Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti na James Gabriel (16), ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana. Tukio hilo lilitokea wakati Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini, Francisco Montecillo Padilla alipokuwa akizindua kanisa hilo. Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne wa Saudi Arabia, na wengine wanne ni raia wa Tanzania
No comments:
Post a Comment