MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Joshua Gitu Mhindi (32), aliyekuwa akikabiliwa na
mashtaka mawili likiwamo la kutaka kumsababishia kifo, Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka.
mashtaka mawili likiwamo la kutaka kumsababishia kifo, Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka.
Mshtakiwa huyo ambaye ni raia wa Kenya aliachiwa na Mahakama hiyo baada ya kuonekana hakuhusika wka namna yeyote kwa mateso ya Dkt. Ulimboka
Hukumu hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Warialwande Lema na mara baada ya kuachiwa polisi walimkamtwa upya baada ya kutuhumiwa kutoa taarifa za uongo kituo cha polisi na shauri hilo lilikuja mbele ya Hakimu Aloyce Katemana.
Shitaka hilo jipya lilisomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, na kudaiwa Julai 3, mwaka jana katika kituo cha Polisi Oysterbay mshitakiwa huyo alitoa maelezo ya uongo kwa maofisa wa polisi
Tarifa iliyodaiwa alikiambia kituo cha polisi hicho kuwa yeye na wenzake ndiyo waliyomteka Dk. Ulimboka
Hata hivyo mshtakiwa huyo alikana shitaka hilo na dhamana yake kuonekana kulegalega baada ya Jamuhuri kuomba kuzuizi cha dhamana
Kwa sababu mshitakiwa huyo hana makazi maalum Tanzania na sababu zingine za kiusalama.
Hata hivyo, Mahakama ilisikiliza ombi la upande wa Jamhuri la kumnyima dhamana mshtakiwa na kurudishwa rumande hadi Agosti 20, mwaka huu.
Mshitakiwa huyo awali alifikishwa Mahakamani Julai 13, mwaka jana akikabiliwa na mashtaka mawili yakiwemo ya kumteka na kumatesa Ulimboka
Dk Ulimboka aliteswa na kutupwa katika msitu na watu ambao bado hawajabainika na kupelekea kupelekwa nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu na sasa amerejea nchini
No comments:
Post a Comment