KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameibua mapya baada ya
kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kusitisha hatua ya Serikali ya kuunda Kamati za Ulinzina Usalama misikitini.
Katika barua yake kwa Waziri Mkuu Pinda aliyoisambaza jana kwa vyombo vya habari, Sheikh Ponda anapinga hatua ya Serikali kuunda mpango huo.
Kutokana na hali hiyo, ameshauri Serikali itoe tamko la kuusitisha mpango huo, ili misikiti iendelee na taratibu zake za kidini na kamati za ulinzi na usalama zibaki katika ngazi ya Serikali.
Amesema Waislamu kama walivyowanajamii wengine, watakapohitaji usalama kwa ajili yao, watafuata taratibu zilizowekwa na Katiba zao na Katiba za nchi na si vinginevyo.
“Sisi kama kikao cha Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, tunapenda kukujulisha hatua tulizochukua kuihami jamii ya kiislamu na madhara ya mpango huu. Tumeiandikia barua hii Serikali itoe tamko la kusitisha mpango wake huu.
“Ieleweke kwamba, Uislamu ni dini huru na uhuru huo unatambuliwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, una fikra, misingi na taratibu zake.
“Mpango huu wa Serikali, umeonyesha dhana ya utumwa na ukandamizaji, kwani inapofikiahatua ya Serikali kuunda mtandaondani ya misikiti unaolenga kuwasimamia maimamu, masheikh, wahadhiri na wasemajiwengine wa kiislamu, waseme nini na waumini wasikilize nini.
“Na endapo watasema kile ambacho hakipendwi na Serikali yako, basi wadhibitiwe na vyombo vya ulinzi na usalama, hatua hiyo ni kinyume kabisa na uhuru wa dini na misingi ya amani na utulivu,” ilisema sehemuya taarifa hiyo.
Sheikh Ponda katika barua yake hiyo, anasema historia inaonyesha kuwa, Tanzania kumekuwa na uvunjaji wa amani na sheria na haki za kiimani ambapo kwa upande wa Waislamu, wanaona huo utakuwani mwendelezo wa historia hiyo ya dola kuvunja haki za kuabudu dhidi yao.
Akitolea mfano, alisema mwaka 1963, Serikali ilipiga marufuku Mahakama ya Kadhi ambacho ni chombo chenye mamlaka ya kutatua mambo ya kiimani na kushughulikia mambo ya ndoa, talaka, mirathi, mali za wakfu, wanawake, malezi ya watoto na usuluhishi.
Alisema kwamba, majukumu hayomsingi wake ni Quran na sunna, lakini pia pamoja na kutambua ukweli huo, Katiba inatamka wazi kuwa, hayo si majukumu ya Serikali, lakini Serikali imeyachukua na kuyakabidhi katika Mahakama.
“Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kupitia Jeshi la Polisi, imeainisha mpango huo ndani ya nyumba za ibada ambapo kwa Waislamu umeanza kutekelezwa kati ya Jeshi la Polisi na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
“Mufti wa BAKWATA, Sheikh Issa Shaaban Simba, alinukuliwa na vyombo vya habari akiishukuru Serikali kwa mpango huo na pia amesema utekelezaji umeanza kwa kusambazwa waraka wa maelekezo katika misikiti yote nchini.
“Ndugu Waziri, sisi Waislamu chiniya kikao chenye hadhi ya mjumuiko wa jumuiya na taasisi za kiislamu, tumeonelea tukuandikie kukueleza kupinga zoezi hilo, kwani linaingilia uhuru wa kuabudu unaohifadhiwa chiniya Katiba ya nchi,” inaeleza barua hiyo.
Aidha, Sheikh Ponda alisema zipo taarifa mpya za hatua za uimarishaji wa mpango huo kati ya BAKWATA na Serikali, ambapo muislamu mmoja alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama Msemaji wa Mufti wa Baraza hilo, akitakiwa aende katika hoteli aliyokuwa amefikia Sheikh Mkuu katika wilaya moja nchini.
Kwa mujibu wa Sheikh Ponda, Sheikh Mkuu aliwahi kufukuzwa katika ngazi ya uongozi wa BAKWATA wa wilaya.
Katika utekelezwaji wa mpango huo kati ya Serikali na BAKWATA, Sheikh Ponda anasema tayari Wilaya ya Namtumbo, Kijiji cha Rwinga, Mkoa wa Ruvuma, Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Smith James, aliitisha mkutano uliohusisha viongozi wa dini na Serikali.
Ameendelea kusema kuwa, katika mkutano huo yalitolewa maelekezo ya Serikali ya kuundwakwa Kamati za Ulinzi na Usalama ndani ya nyumba za ibada.
Katika kikao hicho, Mkuu wa Polisiwa Wilaya (OCD), aliyemtaja kwa jina moja la Mwakasanga, aliwaelekeza viongozi wa dini utaratibu wa kuunda kamati hizo pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe.
“Majukumu ya kamati hizo yaliyoainishwa ni kwamba, kamatiitamhoji muislamu yeyote atakayetaka kuzungumza na Waislamu ndani ya eneo la msikiti na wasiporidhika, watamzuia na kuwasiliana na ofisa usalama wa wilaya.
“Kamati itamhoji sheikh au imamukutoka msikiti mwingine kabla ya kuruhusiwa kuongea na waumini,pia kamati itapitia hotuba ya sala ya Ijumaa katika msikiti husika kabla imamu hajaisoma kwa waumini.
“Kamati za ulinzi na usalama ndizo pekee zitakazokuwa na majukumu ya kuomba kibali serikalini kwa ajili ya mikutano yote ya ndani na nje ya Waislamu na mwisho, aliwaagiza wajumbe wa kikao kuwasilisha taarifa kamili kwa kamati hizo ofisini kwake.
“Mwenendo kama huu, kama tulivyoona katika rejea mbalimbalihuko nyuma, ambao umedumu nakuendelezwa na Serikali za awamu zote nne, kwa kiasi kikubwa umejenga mahusiano mabaya kati ya Waislamu na Serikali,” alisema Sheikh Ponda.
Nakala ya barua hiyo ipo kwa Waziri wa Mamboyandani.
No comments:
Post a Comment