Thursday, October 10, 2013

WAZIRI MKUU, LIBYA ALIVYOTEKWA NYARA LEO ALFAJIRI

Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan aliyetekwa nyara na watu wenye silaha mapema leo alfajiri(10.10.2013)kutoka katika hoteli anayoishi mjini Tripoli
ameachiwa huru. Serikali ya Libya imesema kuwa tukio la kutekwa nyara huenda lilikuwa ni ulipizaji kisasi dhidi ya kitendo cha kikosi cha jeshi la Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mwanaharakati mmoja anayehusika na kundi la al-Qaeda alikamatwa katika mitaa ya mji huo mkuu.
Kutekwa nyara kwa Ali Zeidan kunaakisi udhaifu mkubwa katika serikali ya Libya , ambayo inashikiliwa mateka na wanamgambo , wengi wao wanatoka katika makundi ya wapiganaji wa Kiislamu.
Wanamgambo hao wanasemekana kuwa wamekasirishwa na hatua ya jeshi la Marekani kumkamata mtuhumiwa, anayehusika na kundi la al-Qaeda, ambaye anafahamika kama Abu Anas al-Libi, na wanaishutumu serikali kwa kuruhusu kikosi hicho cha Marekani ama kushirikiana nacho kumkamata mtuhumiwa huyo.

No comments:

Post a Comment