Italia
Katika tukio linalopigiwa upatu kuimarisha hali ya walemavu katika siku za usoni, madaktari huko Italia wameuunganisha mkono huo wa kielektroniki na neva za mabaki ya mkono wa Dennis uliokatwa baada ya ajali mbaya ya fataki na hivyo kumwezesha kuhisi kupitia kwa vidole vya mkono huo wa kielektroniki .
Silvestro Micera aliyeongoza upasuaji huo alifurahishwa mno na uwezo wa mgonjwa wake kuutumia mkono huo bandia .
'' tumeshangazwa sana na urahisi wa mgonjwa wetu kuwasiliana mara moja na mkono huu bandia wa kielektroniki kuekelea majukumu ya kushika na kuhisi vitu tofauti .
Hata ikiwa upasuaji huu utakuwa wa muda tu, ninahakika Denis ameotambua mwenyewe kuwa utakuwa wenye manufaa makubwa kwake katika siku za usoni''
''hisia zangu za mkono zimeimarika maradufu maanake ninawezajua ugumu na mfumo wa kitu chochote ni kama mkono wa kawaida
No comments:
Post a Comment