baadhi waliweza kuswali katika viwanja vya mahakama. |
Mashahidi hao ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Masood Mkome (72), Bakwata pamoja na Meneja Ujenzi wa Kampuni ya Agritanza Limited Hafidh Seiph Othman (42).
Mkome aliulizwa maswali na Wakili wa Serikali Tumaini Kweka kama ifuatavyo:
Wakili: Umekuja mahakamani kuongelea mabadilishano kati ya kiwanja cha Marcus kuwa cha Agritanza, shahidi unakumbuka tarehe mliyobadilishana?
Shahidi: Sikumbuki mwaka wala tarehe kwa sababu siwezi kujua kila kitu.
Wakili:Wewe kama Mwenyekiti mnapata wapi mamlaka ya kiutendaji,na ilikuaje kuhusu eneo la Marcus Chang’ombe?
Shahidi: Tulipata nguvu katika Baraza la Wadhamini la Ulamaa.
Wakili: Mnasema mlibadilishana kwa njia gani?
Shahidi: Muulize Katibu Mkuu Said Loniwa kutoka Baraza la Wadhamini ndiye Katibu Mkuu wa Baraza na ndiye mwenye mafaili yote.
Wakili wa Juma Nasoro wa upande wa utetezi naye alimhoji shahidi kama ifuatavyo:
Wakili: Wewe kama shahidi umewahi kufika katika kiwanja cha Kisarawe mlichobadikishana na Agritanza?
Shahidi: Sijawahi kufika ila kuna baadhi ya watu wa baraza la wadhamini wameenda na siwafahamu kwani kipindi hicho sikuwepo.
Wakili: Je, unao muhtasari wowote au maandishi yanayoonyesha mkataba mlioingia na kampuni ya Agritanza?
Shahidi: Siwezi kujua vitu vipo kwenye mafaili na muhifadhi ni Katibu Mkuu na siwezi kukumbuka kila kitu hata wewe huwezi ila unajua kuuliza tu.
Wakili wa utetezi, Yahaya Njama alipomhoji, shahidi aligoma akidai ni maswali mengi, lakini hakimu alimuamuru ayajibu.
Wakili:Wewe ni kabila gani?
Shahidi: Sisi wote ni Watanzania na usiniulize mambo ya ukabila.
Wakili: Nyie mlikuta kimeuzwa mkamalizia je,wanachama wenu ambao ni Waislamu watawaaminije na wakizuia kuuzwa watakuwa na kosa?
Shahidi aliiambia mahakama kuwa waliopoteza uaminifu hawapo na alipoulizwa swali amekuja kufanya nini mahakamani wakati hajui mshtakiwa wala mshtaki, alidai kuwa alikwenda kutoa ushahidi wa kubadilishana kiwanja.
Shahidi wa pili, Hafidh Seiph alidai kuwa ndiye aliyeenda polisi Chang’ombe baada ya kuvamiwa na kuibiwa.
No comments:
Post a Comment