mkurugenzi wa redio imaan alisema kuwa redio yake ilikua ikiripoti maoni ya watu kuhusu kipengele cha dini kuwekwa kwenye dodosa za sensa. alisema kuwa japo kila mtu ana uhuru wa kuisikiliza redio imaan lkn imewalenga sana waislamu. waislamu ndiyo wenye redio na michango yao ndiyo inaifanya redio iwepo. alisema kuwa waislamu walijenga hoja kuwa wanabaguliwa katika mambo mengi hasa ajira serikalini kwa madai kuwa ni wachache. wao wanaamini ni wengi. walitaka kwenye dodosa kiwekwe kipengele cha dini ili ukweli ujulikane kama zifanyavyo nchi nyingine. alisema kuwa mada ilianzishwa na watu wakawa wanapiga simu kuchangia mada hiyo.
aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi 7 iliyopita, hajawahi kupokea barua kutoka TCRA ikimuonya kuhusu mada ya sensa! inakuaje afungiwe ghafla bila hata karipio!? alisema vipindi vya redio imaan vimekua vikiendeshwa kwa ueledi na kwa kuzingatia taaluma ya utangazaji. redio imaan haijawahi kuhamasisha mtafaruku, kuhatarisha amani na kusababisha vifo vya raia. imekua daima ikieleza na kuripoti ukweli kuhusu mambo mbalimbali yanayotukia hapa nchini.
KATIKA HATUA NYINGINE !
SHEKH MWINGINE AMEKAMATWA MWANZA. NI KUTOKANA NA KAULI YAKE DHIDI YA MAKAFIRI
Sheikh Hamza Omari Amiri wa Umoja wa Vijana wa kiislamu Mkoa wa Mwannza amefikishwa Mahakamani na Kusomewa mashtaka mawili.
La Kwanza Uchochezi kwa kusema Makafiri sasa ni kuwachinja. akiwa msikiti wa thaqib Mwanza.
Pili: Kuwahamasisha waislamu kuwaua Makafiri,
Baada ya hapo Ndugu Yetu Sheikh Hamza Omari Amenyimwa dhamana na kurudishwa rumande hadi tarehe 13-March-2013. vilevile polisi imesema inaandelea kumsaka shekh ilunga kapungu kwa tuhuma za uchochezi.
No comments:
Post a Comment