Monday, February 25, 2013
wakenya:sheria ya ugaidi inavunja haki za binadaam na katiba !
"Hiyo (sheria inayopendekezwa) inamomonyoa haki ya Wakenya ya uhuru wa kujieleza na kukusanyika. Waziwazi inakiuka hata haki za msingi za binadamu."
Zaidi ya watu 200 waliuawa na karibu 5,000 walijeruhiwa mwaka 1998 katika shambulizi la kigaidi ambalo lililenga ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi (shambulizi lililofanyika wakati mmoja na lile lililotokea dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam, Tanzania).
Hali hii ilifuatiwa na tukio la mwaka 2002, ambapo Wakenya 10 na raia watatu wa Israel waliuwa wakati bomu lililotegeshwa ndani ya gari lilipolipuka katika hoteli iliyomilikiwa na raia wa Israel katika mji wa mwambao wa Mombasa. Shambulizi lililoshindwa la kombora lililenga ndege ya abira ya Israel ambayo ilikuwa imeruka kutoka uwanja wa ndege wa Mombasa lilitokea katika siku hiyo.
Matukio yote haya yamekuwa yakihusishwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda.
Muswada wa Kupambana na Ugaidi, uliochapishwa mwaka 2003, una vifungu vya kutaka kuwekwa kizuizini kwa mtuhumiwa wa ugaidi bila kufunguliwa mashitaka kwa muda usiojulikana, na kukamata mali zake – miongoni mwa vifungu vingine.
Ulikataliwa baada ya upinzani mkali kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu, lakini ulikuja kujadiliwa tena Oktoba iliyopita wakati wa mkutano ambao ulihusisha wanaharakati na watalaam wa sheria. Hata hivyo, wanaharakati wanadai sheria hiyo bado inakiuka haki za binadamu – na sasa wanaandaa kuufanya mpango huo kuunganishwa na mkakati wa kiusalama nchini Kenya.
"Tumeamua kwenda hatua zaidi na kuja na mapendekeo yetu juu ya usalama. Ugaidi ni sehemu ndogo tu (ya matatizo ya kiusalama) kwa Wakenya. Tuna tatizo kubwa zaidi la kuongezeka kwa uhalifu," alisema Al-Amin Kimathi, ofisa wa Mtandao wa Haki za Binadamu wa Kenya – chombo mwamvuli cha mashirika ya kutetea haki za binadamu. Mapendekeo hayo, ambayo yataweka kifungu cha kulinda haki, yatapelekwa kwa serikali kwa ajili ya kuzingatiwa.
Pamoja na suala la kuwa na sheria ya kupambana na ugaidi au kutokuwa nayo, mashaka makubwa yanawekwa juu ya watuhumiwa wa ugaidi.
Mwezi Januari mwaka huu, polisi waliwake kizuizini zaidi ya watu 70 kutokana na tuhuma za ugaidi. "Wengi wa watu hawa walibakia kizuizini mwa polisi kwa karibu mwezi mzima, jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Baadhi yao hawakuwa Wakenya; walitengwa, huku ndugu zao wakiwa hawajui walikokuwa," alisema Kimathi.
Kwa sasa sheria inaruhusu mtuhumiwa kushikiliwa kwa muda mrefu zaidi wa masaa 24, au kama ni mtuhumiwa wa makosa ya mauaji, siku 14, kabla hajawapelekwa mahakamani au kuachiliwa huru.
"Hatua za polisi zimesababisha tume kuhisi kwamba serikali inatekeleza Muswada wa Kupambana na Ugaidi kupitia mlango wa nyuma," ilibainisha taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Kenya, chombo kilichoteuliwa na serikali ambacho kina uhuru kamili.
Mashindano ya WCCC yatakayoanza mwezi Machi 24, ambayo yatafanyika mjini Mombasa, yanatarajiwa kukusanya pamoja wanariadha kutoka mataifa 66 ulimwenguni kote.
Mamlaka ya Kenya imekanusha wiki iliyopita kuhusu ushauri juu ya tukio hilo kuwa hauna msingi na ni wa kiunafiki – na kuikosoa Marekani kutokana na kutoa onyo ambalo linaweza kudhoofisha maendeleo ya nchi hiyo.
Zaidi ya hapo serikali imeandikia Shirikisho la Vyama vya Riadha la Kimataifa kulihakikishia kwamba hatua za kiusalama zimeshachukuliwa kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa usalama – hapa ni baada ya shirikisho hilo kutaka ufafanuzi zaidi kuhusu ushauri wa Marekani.
Mwezi Novemba, Marekani ilitoa onyo kama hilo wakati maelfu ya wajumbe kutoka pande mbalimbali ulimwenguni walipokuwa wakisafiri kwenda mjini Nairobi kuhudhuria mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment