Monday, March 4, 2013
AMEDATA NA UNYWAJI WA PETROL
Wahenga hawakukosea waliposema tembea uone na ukishangaa ya Musa utayaona ya firauni, mwanamke mmoja wa nchini Marekani ana mazoea ya ajabu ya kunywa mafuta ya petroli kila siku, kwa mwaka mzima aliofanyiwa uchunguzi alibugia zaidi ya lita 25 za petroli.
Mwanamke wa nchini Marekani aliyejulikana kwa jina moja la Shannon amewashangaza watu wengi duniani baada ya taarifa za tabia yake kupenda kunywa petroli kuandaliwa kipindi maalumu kwenye luninga.
Shannon anakunywa kwa wastani wa vijiko 12 vya petroli kila siku na kwa mwaka mmoja uliopita alikunywa zaidi ya lita 25 za petroli.
Shannon anasema kuwa anajua kuwa petroli ina madhara kwa afya yake lakini ameshindwa kujiuzuia kutokunywa mafuta hayo ya kuendesha magari na badala yake amekuwa akinunua madumu ya mafuta ya petroli na kuyahifadhi nyumbani kwake akijisevia kama vile mtu anavyokunywa maji.
Shannon anapopita karibu na kituo cha mafuta, huuanza kulamba vidole vyake kwa kutamani kunywa petroli.
Madaktari walimuonya kuwa mafuta ya petroli yanasababisha madhara makubwa kwa tumbo, figo na maini huku yakiharibu pia mfumo mzima wa fahamu.
Pamoja na shinikizo la wazazi wake na madaktari, Shannon anapata tabu kujizuia kunywa petroli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment