Hekaheka hiyo ilitokea takriban muda wa saa 3 kupita, baada ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda kuzindua bodi hiyo saa 4.30 asubuhi na kuipa rungu la kufanya mabadiliko kwenye menejimenti ya TBS.
Mwenyekiti wa bodi hiyo mpya, Profesa Cuthbert Mhilu aliwashtua vigogo wa TBS pale alipotangaza kumteua Joseph Masikitiko kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo kwa kipindi cha miezi sita, ambapo Rais Jakaya Kikwete ndipo atatangaza mtu anayetakiwa kuishika wadhifa huo.
“ Tumetekeleza maagizo tuliyopewa, tunataka wakurugenzi mtuletee CV zenu leo. Siku ya Jumatano tutakuwa hapa kwa ajili ya kuwafanyia usaili upya ili kujua kama mnastahili kuendelea kuwapo kwenye nafasi hizo, nawe mkurugenzi unatakiwa kuwafuatilia wakuu wa idara mara moja na kupanga na kupangua,” aliagiza Profesa Mhilu.
Baada ya kutoka kwenye mkutano huo, baadhi ya viongozi walisikika wakilalamika kuhusu bodi hiyo kuamuru kupewa CV hizo jana, huku wakidai kuwa hawakupewa nafasi ya kuziboresha na wengine walionekana dhahiri kutawaliwa na hofu.
Awali akiizindua bodi hiyo, Waziri Kigoda licha ya kuwataka kufanya mabadiliko, pia aliwataka kuvikomesha vikundi vilivyozuka ndani ya shirika hilo ambavyo alieleza vimechangia kulidhohofisha.
“Tambueni kwamba kuna changamoto nyingi, lakini kubwa ni soko letu kuvamiwa virusi vya bidhaa feki. Nimepata taarifa kwamba kuna bidhaa feki kwa asilimia 30, bodi yenu ina kazi kubwa ya kusimamia na kufuatilia masuala ya ubora wa bidhaa zinazolishwa na kuuzwa nchini’’ alisema.
![]() |
CONDOM feki nazo zimekutwa sokoni |
Alisema tatizo ambalo linajirudia sana la betri feki na kwamba linasababisha kelele sana.
“ Tumeshagundua kuwa kuna viwanda bubu maeneo ya Kurasini na kwingineko vinazalisha bidhaa bila vibali wala bidhaa zao hazina nembo. Hivyo Serikali inakosa kodi pia inahatarisha usalama wa watumiaji,” alisema Kigoda.
Aliitaka bodi hiyo kuhakikisha TBS inafanya kazi kwa ushirikiano na Baraza la Taifa la Kutetea Walaji, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na taasisi nyingine zinazohusika ikiwamo Jeshi la Polisi kwa kuwa ni ushirikiano huo ndiyo utakaokuwa na mafanikio.
Alisema TBS inakabiliwa na tatizo la uhaba wa wafanyakazi, ambapo hadi sasa ina wafanyakazi kati ya 400 na 500, tofauti na Kenya ambapo wana wafanyakazi zaidi ya 1,000. Hivyo hata utendaji kazi wao unaweza kwenda pamoja na mahitaji ya ukaguzi unavyotakiwa.
No comments:
Post a Comment