haya ni maeneo ya AKIBA, katikati ya jiji. na taswira ya maji taka. |
MVUA zilizoanza mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es salam zimeshaanza kuonekana kuwa kero kwa wakazi jijini humo.
Mvua hizo ambazo zimeshaanza kuleta adha kwa wakazi zimesababisha barabara kujaa maji na baadhi ya nyumba zilizokuwa mabondeni nazo kupatwa na kadhia hiyo
asubuhi kulishuhudiwa baadhi ya maeneo ikiwemo maeneo ya Kigogo, Tabata watu wamekuwa wakishindwa kuvuka daraja na kulazimika kuvushwa kwa kulipia kiasi cha shilingi 500 ili kuvushwe kutoka ng’ambo moja kwenda nyingine kutokana na maji kujaa
Mvua hizo pia zimeonekana kuporomosha uchumi kwa wafanyabishara kwa kuwa, wafanyabiashara hao wamelalamikia mvua hizo zinaporomosha mapato kwakuwa wanunuzi kutofika kununua bidhaa kutokana na hali hiyo
No comments:
Post a Comment