Wednesday, March 13, 2013

MTIKILA mbaroni, anawataka wakristo wapambane na waislamu.


jeshi la polisi mkoani Rukwa nchini Tanzania limemkamata na kumhoji Mwenyekiti wa chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila kwa tuhuma ya kuhusika na uchochezi wa kidini dhidi ya Waislamu.
mch. mtikila akiwa na gazeti huku akisistiza jambo.
Mtikila ambaye kwa sasa ameachiliwa huru kwa dhamana wakati uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo ukiendelea, yuko mkoani Rukwa kwa takribani wiki mbili sasa na alikamatwa mwishoni mwa wiki hii. Inadaiwa kuwa Mtikila aliitisha kongamano la wachungaji na viongozi wengine wa Kikristo katika ukumbi mmoja mjini Sumbawanga na kuwachochea kupambana na Waislamu.

Kamanda wa polisi mkoani Rukwa, Jacob Mwaruanda, amesema kuwa katika kongamana hilo Mchungaji Mtikila aliwaeleza viongozi hao kuwa wamekuwa wakionewa na Waislamu kutokana na matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea nchini Tanzania hivi sasa. Mwaruanda alisema katika kongamano hilo mchungaji huyo anadaiwa kuwahamasisha Wakristo kuwavamia Waislamu kwa madai kwamba Waislamu wanawaonea Wakristo.



Akihojiwa na Polisi Mch,Mtikila alisema kwamba yeye akiwa kama Mwenyekiti wa Amani kwa Wachungaji wote Tanzania, anayo haki kupinga na Kujadili swala la Dini Moja [Waislamu] kuwanyanyasa watu wa Dini nyingine kwa Kuwaua Viongozi wake na Kuchoma Makanisa!!
inadaiwa kuwa Mtikila pia alielezea suala la uchinjaji wa ngombe kuwa ni miongoni mwa mbinu za waislamu za kutoka kudhoofisha ukristo nchini.
Hata hivyo Mch,Mtikila aliachiwa kwa Dhamana baada ya kushikiliwa kwa muda na Kuhojiwa!!


awali mchungaji huyu alihawahi kufishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam mbele ya Hakimu Michael Mteite kwa kosa la uchochezi na kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. ambapo Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mnamo tarehe 1 Novemba, na tarehe 17 Aprili, Mchungaji huyo alitamka kuwa “Kikwete anataka kuangamiza Ukristo” na kudai kuwa Wakristo wasipoangalia Ikulu wataisikia kwa jina tu. Katika kosa la pili mnamo tarehe 16 Aprili katika eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, Mtikila alikutwa na nyaraka za kumkashifu Rais Kikwete, jambo ambalo ni kosa kisheria.

No comments:

Post a Comment