Wednesday, March 13, 2013

marekani, KUZIFUTA NDOA ZA MASHOGHA, ni baada ya kuonja madhara yake.


Mwaka 1996 Sheria ya Ndoa za Jinsia Moja ilisainiwa na  aliyekuwa Raisi wa 42 wa Marakeni Bill Clinton ijulikanayo Kama Defense of Marriage Act a.k.a DOMMA.

Siku chache zilizopita Raisi huyu amaiomba Mahakama Kuu nchini Marekani kuifuta Sheria Hii kwa sababu ya Mapungufu Mbali Mbali yaliopo kwenye hii Sheria.

Raisi huyu Ameendela kueleza kwamba kwenye Sheria ya Ndoa ijulikanayo kama DOMA (Defense of Marriage Act )kusema wazi kwamba ndoa ni Muunganiko kati ya Mwanamke na Mwanaume tu na sio zaidi ya Hapo.Lakini zaidi ya hapo Mahakama Kuu ya Marekani imesema itatoa maamuzi yalio rasmi kisheria
mwezi Juni mwaka huu kuhusu ndoa za jinsia moja.

Majaji wataamua kama Defense of Marriage Act kama inashabiliana na kanuni za Taifa linaloheshimu uhuru ,usawa na haki kwa ujumla na ambazo hazipingani na Katiba Mama ya Nchi Ya Marekani.

Raisi huyo aliendelea kusema kwamba Wakati anapitisha Sheria hiyo Ulikuwa ni wakati tofauti na Sasa sababu hakuna hata jimbo moja lililokuwa linatambua ndoa za jinsia mmoja lakini majimbo mengine yilikuwa yinafikiria kufanya hivyo na wengi walikuwa wanataka mabadiliko ya haraka.Kwa Mfano Mpaka  kufikia sasa Majimbo zaidi ya Tisa ikiwemo Colombia District watu wenye mahusiano ya jinsia moja hawewezi kupatiwa huduma za kajamii kama ilivyo kwa watu wenye mahusiano ya jinsia tofauti…..USA Today ndio limeripoti .

No comments:

Post a Comment