Friday, May 3, 2013

Rachid Nekkaz: acheni allah aabudiwe,vaeni nikkab,ntawalipia faini zote.

pichani ni Rachid Nekkaz,huyu ni mfaransa mwenye asili ya algeria ambaye kwa sasa anaishi nchini
ufaransa. leo namtambulisha kwenu kwa sababu moja, nchini ufaransa serikali iliamua kupiga marufuku uvaaji wa hijabu kwa wanawake katika hadhara ya watu kinyume na sheria ya kiislamu na maadili yake kwa wanawake. hatua hii iliambatana na dola hiyo dhalimu kulifanya jambo hilo kuwa kitege uchumi cha nchi hiyo kwani akikamatwa aliyevaa hijabu hadharani analazimika kulipa faini. alhamdulilah allah alimuelekeza mja wake huyu kujitolea katikamapato yake ya halali kuwa
atawalipia wanawake faini zote hivyo wasitishike kabisa na kuacha kuacha kutekeleza amri ya allah subhanahu wata'ala. ameanzisha mfuko maalum kwa kazi hiyo ambapo kwa kuanzia ameweka kiasi cha paund milioni moja kwa ajili ya kuinusuru jamii ya wanawake wa kiislamu kote ulimwenguni ambako dola hizi dhalimu zitaanzisha utaratibu huu mchafu na haramu. na katika picha hiyo alikuwa amekwenda kulipa faini hizo katika mamlaka ya matapo ya ufaransa. shime waislamu matajiri hasa wanaotokea katika nchi zinazoitwa eti ni maskini. jitoleeni kwamali zenu kuhamasisha utekelezaji wa sheria za allah katika jamii zetu.

No comments:

Post a Comment