Kiongozi wa Salafist Ansar al-Sharia |
miongoni mwa makundi ya kigaidi.
Kundi hilo linatuhumiwa kuhusika na mauaji ya wanasiasa wawili walio na siasa za wastani.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Ali Larayedh, amesema ana ushahidi wa kutosha kuthibitisha, mauaji ya Chokri Belaid na Mohamed Brahmi, ambayo yalisababisha machafuko ya kisiasa nchini humo, yalitekelezwa na kundi hilo.
''Mtu yeyote ambaye ni mwanachama wa kundi hilo ni lazima akamatwe na kufunguliwa mashtaka'' Alisema waziri huyo.
Kundi hilo ambalo liliundwa baada ya mageuzi ya kisiasa ya mwaka wa 2011, linataka sheria za Kiislamu maarufu kama Sharia kuanza kutumika nchini Tunisia.
Bwana Larayedh, amesema pia kundi hilo linaunga mkono kundi moja la Kiislamu ambalo limekuwa likisakwa na wanajeshi wa nchi hiyo kwa miezi kadhaa, katika maeneo ya milima ya Chaambi karibu na mpaka wa nchi hiyo na Algeria.
Jeshi la nchi hiyo lilianzisha mashmabulio makali dhidi ya kundi hilo mwezi uliopita baada ya wanajeshi wake wanane kuuawa na wapiganaji wa Kiislamu walio na uhusiano na kundi la kigaidi la al-qaeda.
No comments:
Post a Comment