Rais wa Liberia, Ellen Sirleaf Johnson |
- NI AGIZO LA RAIS sirleaf....
Rais wa Liberia, Ellen Sirleaf Johnson, amesema chuo kikuu kinachomilikiwa na serikali, kimekubali kuwasajili wanafunzi elfu moja mia nane ambao walifeli mtihani wa mwisho wa kitaifa wa shule ya upili.
Raos Sirleaf amesema kuwa ameshauriana na maafisa wakuu wa chuo hicho kuhusiana na suala la wanafunzi wote waliofeli.
Takriban wanafunzi elfu ishirini na tano waliotahiniwa walianguka mtihani huo, huku maafisa wa elimu wakisema wengi wao hawana ufahamu wa lugha ya Kiingereza.
Rais huyo amesema kuwa, wasimamizi wa chuo hicho waliweka viwango vya kufuzu kuwa juu zaidi, na hivyo kuwafungia wanafunzi wengi nje.
Hata hivyo hakusema, kwa nini chuo hicho kilichoko mjini Monrovia, kimekubali kuwachukua wanafunzi elfu moja mia nane, baada ya mashauriano naye.
Akijibu wakosoaji wake ambao wanadai kuwa ameshindwa kuimarisha viwango vya elimu nchini humo tangu mwaka wa 2005, wakati alipochaguliwa kuwa rais, Bi. Sirleaf alisema'' Kwa hakika wao hawana msingi wowote, hakuna njia ya mkato kwa sasa''.
''Idadi ya wanafunzi waliojiunga na shule tangu nilipochaguliwa imeongezeka maradufu'' Alisema Bi. Sirleaf.
No comments:
Post a Comment