Zaidi ya Sh41.4 bilioni zimepatikana kutokana na malipo ya huduma za Mkongo wa Taifa (NICTBB), ambapo hadi Agosti mwaka huu, kampuni 16 zikiwamo 9 za nje zimeunganishwa kwenye mtandao huo imara kwa mawasiliano.
Pia mipango inafanywa kuunganisha vituo vya runinga na redio kwenye huduma hiyo. Hayo yamebainishwa juzi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL),Kamugisha Kazaura, katika taarifa yake aliyoitoa kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu.
Alieleza kuwa ni kampuni saba pekee za ndani zilizounganishwa na NICTBB,
alizitaja TTCL yenyewe yenye jukumu la kusimamia mkongo huo, mengine ni Zantel, Simbanet, Airtel, Tigo, Infinity Africa na Vodacom.
Kampuni za nje ni pamoja na MTN-Zambia hadi Malawi, MTN–Rwanda, Airtel Rwanda, KDN, RDB, Econet, BCS na UCOM-Burundi.
No comments:
Post a Comment