Tuesday, October 29, 2013

wabunge wamkomalia makinda na ndugai

Leo katika kikao cha kawaida cha kupeana taarifa za mambo mbalimbali ya bunge, wabunge wamemjia juu Spika Anna Makinda na Naibu Spika wake Ndg Job Ndugai wajiuzulu kwa kushindwa kusimamia kanuni ipasavyo na pia kwa kushindwa kusimamia maslahi ya wabunge.


Katika kikao hicho hoja ya kudai pensheni ya wabunge ilianzishwa na Mhe Kombo Khamis Kombo wa CUF na baadaye Mhe Hamis Kigwaangala wa CCM akaiweka sawa na kutoa hoja ambayo iliungwa mkono na wabunge wote kuwa sheria ya national assemply ya mwaka 2008 inayoelekeza na kusimamia maslahi ya wabunge itekelezwe ipasavyo na kwamba mfuko wa bunge utoke katika kusimamiwa na ofisi ya waziri mkuu na badala yake usimamiwe moja kwa moja kutokea hazina kuu na kwenye bajeti muwasilishaji awe ni Naibu Spika ili ahojiwe na wabunge badala ya serikali.

Hii italifanya bunge kuwa huru na kufanya mambo yake ipasavyo. Mbali na hili Kigwangala alitaka kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mh ANdrew Chenge wa CCM Bariadi ivunjwe kwa kuwa imegubikwa na tuhuma za ufisadi kwa kujilipa posho ya siku moja ya sh 430,000 na akatolea mfano wa double payment wakati wa kikao cha bunge kwamba walikuwa wanalipwa posho za vikao viwili, cha bunge na cha bajeti wakati kamati nyingine zote zikifanya kazi wakati wa bunge huwa hazilipwi posho nyingine ya pembeni.

Wabunge wengi walimuunga mkono kwa kushangilia na kumtaka atoe hoja, ambayo aliitoa na ilikubaliwa. Mh Tundu Lissu naye alimuunga mkono na kusisitiza kuwa Mh Chenge kama ana heshima basi ajiuzuru mwenyewe kwa kuwa hakuna kiongozi wa bunge anayeteuliwa. Alisema 'viongozi wote wa bunge, kwa kuwa bunge ni taasisi ya kidemokrasia, huwa wanachaguliwa na wenzao, sasa iweje yeye akubali kuteuliwa wakati ni mwanasheria aliyebobea na anajua utamaduni wa mabunge?'

Pia kuhusu maslahi ya wabunge alidai yanalindwa na sheria ya national assembly na kwamba Rais ndiye anayeamua kuhusu mafao ya wabunge na maslahi yao kwa ujumla hivyo kujadili mambo haya hapa tunapoteza muda. Mh Kangi Lugola wa CCM Mwibara naye alitoa hoja ya kuwataka wajumbe wa tume ya utumishi ya bunge waende mbele na Mh Vuai Nahodha (aliyekuwa akiongoza kikao atoke mbele) awapishe viongozi wa tume na Spika na Naibu Spika wakae pale mbele wajibu hoja za wabunge vinginevyo waajiuzuru wenyewe kabla hatuwajawatoa.

No comments:

Post a Comment