Kwenye kongamano hilo ambalo masheikh mbalimbali wakiwemo Sheikh Ponda Issa Ponda, Ally Basaleh, Mussa Kundecha na Kondo Juma Bungo waliwasilisha mada mbalimbali pamoja na kutangaza maazimio ya kongamano hilo.
Moja ya mambo yaliyozungumzwa ni mapendekezo waliyowasilisha kwenye Tume ya katiba mpya ambapo
Hoja hiyo ilikuja baada ya kunukuliwa kauli ya Waziri wa nchi Sera na Uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi, wakati akijibu swali la Mbunge Asumta Mshama aliyetaka kujua kwamba lini serikali itaacha kupanga siku ya kupiga kura kuwa Jumapili wakati wanajua siku hiyo ni siku ya ibada ya wakristo haioni inawadhulumu hakiyao yakufanya ibada?, Lukuvi kwenye jibu lake alisema suala hilo limekuwa likilalamikiwa na watu wengi tu lakini serikali kwenye hilo haina utaratibu maalum wa siku ya kupiga kura ila kwakuwa kuna mchakato wa katiba mpya hilo litazingatiwa.
“Hii ni kinyume kabisa na utaratibu wa tume ya katiba waziri huyu anataka tuamini kwamba anayafahamu yatakayokuwemo kwenye katiba mpya kabra hata wananchi hawajapelekewa na hata haijaandikwa? Hivyo iweje waisilamu wanaodai siku ya ijumaa iwe ya mapimziko kwa miaka nenda rudi hawapewi wakristo wanakosa sikumoja tu ndani ya miaka mitano majibu yanapatikana kirahisi?” Alihoji sheikh Ponda.
“Waisilamu wamekuwa wakiomba ruhusa kwa mabosi wao siku ya ijumaa kwenda kufanya ibada na mara nyingine wananyimwa ruhusa hiyo lakini hakuna vurugu yeyote waliofanya na wanadai haki hiyo kwa miaka yote hii lakini hawapewi lakini wengine wanadai kirahisi na kujibiwa kwa uhakika.” Alifafanua.
katika kupigania haki za waislamu hatutarudi nyuma mpaka tone la mwislamu wa mwisho. na tuko tayari kumsikiliza shekh ponda sasa. takbiiirrrrr wakaitikia wote allahu akbarrrrrrrrr!!!!! |
Aidha heikh Ponda alifafanua kuwa waisilamu wavumilie wasubiri rasimu itakapotangazwa kwenye magazeti ya serikali kama mapendekezo waliyowasilishwa yatapuuzwa basi hakuna katiba mpya maandamano usiku na mchana mpaka kieleweke nchi nzima. katika hatua nyingine shekh ponda alizungumzia kidogo kuhusu mambo ya mtwara akisema serikali dhaifu imekurupuka nakwenda kuwafanyia unyama wa kutisha waislamu wa mtwara na akilinganisha na mgogoro wa ardhi wa loliondo ambapo anasema wote hawa ni raia na wote wanapigania rasilimali ya taifa lao waliopewa na mungu nawala si mali ya serikali walachama tawala. vile vile aliwataka waislamu kutambua kuwa wao wamekuwa watanzania si tu kwakutambuliwa na sheria ya bunge wala katiba ya nchi. wao ni watanzania kwa sababu allah ndiye aliyewaumba katika ardhi hii ya tanzania na hivvyo wasikubali kuona wanapokonywa uhuru wao kwa namna yoyote ile....
Sheikh Konda Juma Bungo nae aliwasilisha mada. |
No comments:
Post a Comment