Friday, February 7, 2014

JK: bunge la katiba limeiva

Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa Bunge Maalumu la Katiba litaanza Februari 18 mwaka huu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuweka mbele masilahi ya Taifa na siyo ya vyama vyao.
Rais Kikwete alisema wajumbe 640 wa Bunge hilo wengi ni wafuasi wa vyama vya siasa, hivyo wanatakiwa kukubaliana kwa hoja badala ya kila upande kuvutia kwake.

#liz huenda akatendewa "HAKI"

Msichana aliyebakwa na genge la watu sita nchini Kenya hatimaye huenda akapata kutendewa haki.
Liz mwenye umri wa miaka 16, alibakwa na kujeruhiwa vibaya mwezi Juni baada ya kutupwa ndani ya shimo la choo katika jimbo la Busia Magharibi wma Kenya.

waislamu waihama CAR. wahamia cameroon, chad.

Maelfu ya waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakiondoka katika mji mkuu wa taifa hilo Bangui mapema leo.

Wakiwa wameabiri malori na kusindikizwa na wanajeshi wa taifa la Chad,ni msafara wa hivi karibuni wa waislamu kutoroka vita wakiwa na matumaini ya kupata hifadhi katika taifa jirani la Chad.

Thursday, February 6, 2014

UKATILI...

Wanajeshi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamemuua mwanamume mmoja anayetuhumiwa kuwa muasi huku ghasia zikiendelea kukithiri nchini humo.

wakana kuwepo kwa #kiinua_mdomo.

Serikali  imekanusha taarifa za vyombo vya habari zilizodai kuwa wabunge wa nchi hiyo watalipwa kiasi cha zaidi ya dola laki moja za kimarekani watakapomaliza muda wao wa kipindi cha miaka mitano yakiwa malipo ya #kiinua_mdomo.
Taarifa ya wizara ya fedha imesema habari hiyo ni ya upotoshaji kwa kuwa Waziri wa fedha ,hakuwahi kuzungumza na mwandishi yeyote kama inavyodaiwa kuwa alithibitisha taarifa hizo.

Wednesday, February 5, 2014

"unga" wa mabilioni ndani ya JAHAZI la iran

picha kwahisani ya BBC.
Polisi nchini wamekamata shehena ya dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa kilo 201 katika eneo la bahari kati ya Dar es Salaam na Zanzibar 

mkono wa Kielectroniki

mlemavu mmoja kutoka Denmark Dennis Aabo amekuwa binadamu wa kwanza kupewa mkono wa kieletroniki wenye hisia kama ule wa binadamu.

Gavana awaomba radhi wanawake

Mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya amewaomba radhi wanawake kwa matamshi yake wiki jana kuwa wanawake ambao hawajaolewa hawapaswi kushikilia nyadhifa za kisiasa.
Gavana wa kaunti ya Kiambu nje kidogo ya Nairobi, William Kabogo, amesema kuwa ikiwa wanawake wana umri wa miaka 35 na bado hawajaolewa basi wao sio timamu.

Monday, February 3, 2014

MTIKILA ASHABULIWA, ni mgogoro wa ardhi

Kiongozi wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amenusurika kifo na mtu mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Mikidadi, ambaye yupo mahututi katika Hospitali ya Temeke, baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa na mzozo wa ardhi eneo la Kurasini, jijini Dar es Salaam.

Thursday, October 31, 2013

wabunge wadai posho zao ni ndogo, waomba nyongeza

WAKATI watumishi wa umma wakitaabika na mishahara midogo, huku wakipendekeza marupurupu ya wabunge yapunguzwe, wabunge wa CCM juzi waliwaweka kitimoto viongozi wa Bunge wakitaka mishahara yao ipandishwe.

wizara yafuta div zero kwa matokeo ya sekondari nchini,


Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi.

Tuesday, October 29, 2013

waislamu 3 wanaompinga kikwete wauwawa ,kilindi-tanga


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa,Aliwataja wafuasi waliouawa kuwa ni Ramadhan Hamis, ambaye ni mfanyabiashara wa madini na mwingine jina lake halikufahamika mara moja lakini inasemekana ni mwalimu wa dini ya Kiislamu (ustaadh) Kijiji cha Lwande.

wabunge wamkomalia makinda na ndugai

Leo katika kikao cha kawaida cha kupeana taarifa za mambo mbalimbali ya bunge, wabunge wamemjia juu Spika Anna Makinda na Naibu Spika wake Ndg Job Ndugai wajiuzulu kwa kushindwa kusimamia kanuni ipasavyo na pia kwa kushindwa kusimamia maslahi ya wabunge.

Monday, October 28, 2013

RAIS ATOA POLE KWA MAMA WEMA SEPETU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma, leo wamehudhuria msiba wa baba yake na muigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu, Balozi Abraham Sepetu aliyefariki jana baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya kisukari na kiharusi. Alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam..

dawa za kulevya:Viongozi wa dini wametaja majina 61 ya vinara,

Viongozi wa dini wametaja majina 61 ya vinara wanaojihusisha na dawa za kulevya nchini ambao wanatarajia kuwaburuza katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), mjini The Hague, Uholanzi kujibu tuhuma zao.